Saturday, October 26, 2019

JINSI YA KUTUNZA UPENDO NA URAFIKI KATIKA MAHUSIANO YA KIMAPENZI

Watu Wengi Ambao Wako Kwenye Uhusiano Wanalalamika Kuwa Wenzi Wao Hawawaoneshi Upendo Kama Ilivyokuwa Siku Za Mwanzo Za Uhusiano Wao. Wanaeleza Kuwa Wanaona Uhusiano Wao Unalegalega Na Mapenzi Yanapungua Taratibu Kama Barafu Iyeyukavyo Juani.
Ili Kuepuka Yote Haya, Hauna Budi Kujifunza Njia Za Kuwasha Upya Moto Wa Upendo Kila Wakati Kwa Kuongeza Ukaribu (Intimacy) Kati Yako Na Mwenzako.
Zifuatazo Ni Mbinu Zitakazokusaidia
1. Kucheka Pamoja na mpenzi wako
Kicheko Ni Mlango Wa Ukaribu, Kama Mwaweza Kucheka Pamoja Basi Mwaweza Kulia Pamoja, Na Hapa Mwaweza Kuaminiana Zaidi Katika Kuwasiliana Hisia Zenu, Kama Waweza Kuitofuta Furaha Katika Kila Kitu Basi Unaweza Kupenya Katika Vyote. Usiwe Mgumu Na Mwenye Msimamo Mkali Katika Kila Kitu. Jifunze Kujizuia Pale Unapoanza Kuelekea Kwenye Kukasirika Na Badala Yake Tumia Kucheka Kama Mlango Wa Kutokea. Kama Utaanza Kujizoeza Hivi Ukiwa Nyumbani, Taratibu Utaweza Ukiwa Ofisini Na Hata Kwingine Kokote.
2. Kutiana Moyo na mpenzi wako
Kila Mmoja Awe Msaada Na Tegemeo Kwa Mwenzake. Jifunze Kumtia Moyo Na Kumwezesha Mwenzako. Sikiliza Na Kufuatilia Vile Mwenzako Afanyavyo Au Apendavyo.
Onyesha Heshima Katika Vitu Hivyo Pia. Kila Upatapo Nafasi Mpongeze Mbele Za Watu Au Hata Unapokua Nae Peke Yenu. Mjenge Mwenzako Mbele Ya wengine Na Kubali Pongezi Zote Za Mafanikio Yenu Zimwendee Yeye. Mruhusu Mpenzi Wako Ajue Kuwa Una Mkubali Katika Kila Afanyalo. Zaidi Tunavyo Wainua Wapenzi Wetu Ndivyo Wanavyotuthamini Na Kutunyanyua Na Sisi Pia.
3. Kupenda Kugusana na mpenzi wako
Nguvu Ya Mguso Wa Ukaribu Kamwe Haiwezi Kulinganishwa Na Chochote. Lazima Mjifunze Kujenga Tabia Ya Kugusana Mara Mpatapo Nafasi Sio Tu Mnapokuwa Mmelala. Kugusana Huku Ni Pamoja Na Kushikana Mkono Mkiongea Au Mkitembea, Kukumbatia Bega, Kugusa Au Kuchezea Nyewele Za Mwenzako Na Njia Nyingine Zozote Za Kuonyesha Ukaribu Kimwili. Wengi Wetu Huweza Kufanya Haya Kidogo Tunapokuwa Peke Yetu Na Kamwe Sio Mbele Ya Watu, Je, Ni Aibu, Nidhamu Mbaya? Dhambi?
Kugusana Ndiyo Mwanzo Wa Kuamsha Hisia Za Kuhitajiana, (Hebu Jiulize Kisirisiri, Lini Uligusana Na Mwenzako Nje Ya Chumba?). Kumgusa Umpendaye Hukuzuia Kutowaza Kumgusa Yeyote Katika Ulimwengu Uliojaa Wengi Walio Wapweke.
Mguso Huu Wa Upendo Haumaanishi Mguso Wa Tendo La Ndoa, Ingawa Pia Ni Vyema Kujifunza Kuijenga Lugha Ya Mguso Wa Tendo La Ndoa Katika Uhusiano Wenu.
4. Zungumza Hisia Zako na za mpenzi wako
Kati Ya Vikwazo Vikubwa Katika Ustawi Wa Uhusiano Mengi Hususan Ya Wanandoa Ni Kutokuwepo Kwa Majadiliano. Lazima Wapenzi Wajifunze Kuzungumza Kuhusu Hisia Zao. Kama Vile Maisha Yasivyo Na Ukamilifu, Uhusiano Na Hata Ndoa Pia Hazina Ukamilifu. Mpenzi Wako Hayuko Kamili Na Wala Wewe Pia Siyo Mkamilifu. Jifunze Kuzungumza Na Umpendaye Jinsi Unavyojisikia Na Nini Kinachokusumbua. Kuendelea Na Migogoro Isiyosuluhishwa Husababisha Moyo Kuwa Baridi Juu Ya Mwenzako. Jiwekeeni Muda Kila Wiki Wa Kutoka Ili Kuzungumza Mambo Yenu. Mwambie Umpendaye Yapi Yanayojiri Kila Siku Na Zipi Ni Changamoto Zako Mkiweza Kujifunza Kuwekeza Katika Muda Wa Kuwa Pamoja Taratibu Hata Muda Wenu Wa Maongezi Ya Simu Utaongezeka.
5. Msamehe mpenzi wako Na Kubali Kusamehewa naye
Kamwe Tusiache Maumivu Na Machungu Yatawale Uhusiano Wetu. Lazima Tujifunze Kuwasamehe Tuwapendao Na Kujisamehe Sisi Pia. Kutofautiana Katika Uhusiano Kupo Sana, Na Lazima Tuwape Tuwapendao Nafasi Ya Kuelezea Vile Vinavyowaudhi Dhidi Yetu. Kila Hisia Za Mmoja Wetu Zina Umuhimu. Huwezi Kujiona Vile Ulivyo, Mruhusu Mwenzako Akwambie Yanayomuumiza Na Msameheane.
6. Linda Mwonekano Wa Mpenzi Wako
Mara Nyingi Hatari Hii Hutokea Tunapokuwa Katika Mizunguko Ya Huku Na Huko. Ukaribu Na Mpenzi Wako Hauendelezwi Tu Bali Unalindwa. Mwonekano Wetu Lazima Uwe Halisi Na Siyo Bandia . Vile Tunavyoviona Katika Tamthiliya Na Filamu Siyo Ukaribu Ulio Halisi. Kama Tunataka Tuonekane Sawa Na Vile Tunavyowaona Wengine Wanavyopendana Basi Tunakosea Na Kujizuia Kuwa Na Mtazamo Bora Katika Uhusiano Wetu. Ukianza Kupata Ukaribu Wa Kweli Baina Yako Na Mwenzako, Utapoteza Hisia Ya Kuhitaji Ukaribu Huo Na Mwingine Yeyote, Na Badala Yake Utaanza Kuulinda Ukaribu Mlionao.
Lengo Liwe Kuvitafuta Vile Vyote Mpenzi Wako Alivyonavyo Ambavyo Ni Kukuza Ukaribu Wenu. Mwenzako Awe Ndiyo Mtu Wa Muhimu Kuliko Wote Katika Maisha Yako.

Saturday, October 19, 2019

MANENO MATAMU KWA MWENZA WAKO


Malkia wangu, kipenzi cha moyo wangu.
Asante kwa kuja kwenye maisha yangu, na kunipa furaha na upendo uliobadilisha maisha yangu.

Kamwe siwezi usahau umuhimu wako kwangu.
Na jinsi unavyonifanya nijione mwenye bahati na nimebarikiwa kushinda yeyote yule.

Sijutii kukufahamu, sijutii kuwa wako, sijutii kukupenda, na popote nilipo najivunia kuwa wako na sitachoka kuzisema sifa zako.

Babe,
Tunaishi kwenye dunia yenye watu zaidi ya billion 7, lakini bado nafsi yangu, akili yangu, macho yangu, na moyo wangu viko kwako mrembo uliyeteka hisia zangu.

Ni wewe tu unifanyae nijihisi nimekamilika kwajinsi unavyonikubali na kuyavumilia madhaifu yangu pasipo kuchoka.
Ni wewe pekee unifanyae nihisi dunia nzima iko kiganjani mwangu, kwajinsi unavyo niheshimu na kunithamini.

Nakupenda,
Nakupenda my love na sitamani kuwa mbali nawe.
Nakupenda sana kipenzi changu, and you mean everything to me.

Honey
Nitazidi kuwa mume mwema kwako, na kuhakikisha nalilinda tabasamu lako.
Nitasimama nawe na kukusupport mpaka utimize ndoto zako.
Nitakulinda na kukupa heshima na upendo ambao Malkia wangu unaustahili.

Babe you're so damn beautiful, najisikia raha kukutazama kwajinsi unavyonivutia😍

I love you, take care sweetheart 😘😘😘
***********

Kama leo hujamwambia maneno mazuri mpenzi wako, mumeo or mkeo.
Basi usiiache siku ipite bila kumwambia maneno mazuri.
Mwambie unampenda na unathamini kiasi gani uwepo wake kwenye maisha yako.

Unaweza hisi ni ujinga, lakini always maneno matamu yatokayo kwako kwenda kwa akupendae.
Huwa yana maana kubwa sana kwake, na yatampa furaha na kumfanya ajihisi dunia yote ni yake.


Friday, October 18, 2019

MPE MDA WAKO


Upo nae basi MPE nafas ya kuwa nae,usijifanye upo bize sana wakat anataka mda wako.Kwa nini uwe bize na simu yako au TV wakat MWenzako anakutaka we?

Sawa kuna mda wa kuwa bize na kazi lakin jitahid japo uendapo kupata chai au chakula mtumie hata SMS fupi " NIME KUKU KUMBUKA SANA MY LOVE...."

Lin atacheka nawe
Lin ambapo atacheza nawe?

MPE mda wa kutosha
Aondokane na upweke!!!!!!

Monday, October 14, 2019

JINSI YA KUMFANYA MWANAMKE AWE NA FURAHA





Kila mwanaume anapenda kujua jinsi ya kumchangamsha mwanamke ili ampende. Lakini wengi hushindwa njiani pale wanapojaribu kufanya hivyo kwa sababu hawajui vitu vitano vya kumchangamsha mwanamke.

Yafahamu hayo mambo matano, na namna kuyatumia.

Nadhani utakuwa ushashuhudia baadhi ya wanaume wakichati na wanawake(zao),wakati mwingi unakuta mwanamke anacheka na kumsifia kuwa anamfurahisha(“hahahaha!…. unanifurahisha”).

Kuambiwa na msichana kuwa unamfurahisha ni mojawapo ya kitu kikubwa sana ambacho wanaume wengi hawakisikii kutoka kwa mwanamke. Haihusiani na muonekano wako, ila namna unavyopangilia hoja zako na mada zako kwake na jinsi unavyoziwasilisha kwa kuangalia mazingira.

Jinsi ya kumfurahisha na kumchangamsha mwanamke
Ni kitu gani hasa kinamfurahisha mwanamke? Hauwezi kumfurahisha mwanamke kwa kumkejeli au kumshika baadhi ya maeneo ya mwili wake(utaishia kumchukiza na kujiondolea point).

Utajua unamfurahisha mwanamke pale tu unapomfanya ajisikie furaha, na wakati mwingine hushindwa kujizuia na hujikuta anakukiss!.

Ntakupa mambo matano ya kufanya ambayo yakuufurahisha moyo wa msichana unayemtaka(kumpenda).

Unaweza kubadilisha muonekano wako kimavazi, wakati mwingine unaweza kumkazia macho lakini hiyo haitamfurahisha bali itamtisha.

Kumchangamsha/kumfurahisha mwanamke kunahitaji kutengeneza mvuto(impression) zaidi ya muonekano na swaga.

Kama unataka kujua jinsi ya kumfurahisha mwanamke , mwanzo wa yote, huanza na maongezi. Na mwisho wa yote ni hapo pia.

Mawasiliano mazuri kimaongezi ndiyo njia pekee ya kumfurahisha na kumchangamsha msichana.

Yatumie haya mambo matano, na utafanikiwa hata kabla ya kufikia mwihso:

1. Mshawishi kupitia kitu anachokipenda
Unaweza kudahani hii haina umuhimu. Wanaume wengi hufikiri hivyo na hushangaa kwanini tu niongee kuhusu kitu ambacho msichana anakipenda. Kwanini wasichana nao wasiongee kuhusu vitu wanavyovipenda wanaume?

Wanawake huweza kufanya hivyo, japo hatujui. Wanawake wengi hujitahidi sana kujua wavulana hupenda kuongelea nini. Lakini, wakati unataka kumvutia msichana, ni muhimu ukajua ni kitu gani kinachoendelea kwenye mawazo yake. Sasa tambua kwamba, kujua kitu msichana anachokipenda haimaanishi, dhahabu, mitindo au vipodozi. Tofauti kati ya msichana na mvulana kwa namna ya kuishi imepungua sana kwa sasa(wanawake hufanya vingi ambavyo wanaume hufanya). Kwa maana hiyo ni rahisi kuwa na maongezi yenye kuvutia bila kuboa. Achana na mambo ya mahesabu, michezo, teknolojia, amini yatakua poa tu maongezi yenu.

2. Mtanie
Unapoongea na msichana, ni rahisi sana kumfanya na yeye aongee na wewe hatakama hakupenda mwanzo. Lakini hiyo haitoshi. Kama unataka kujua ni jisi gani ya kuongea na msichana/mwanamke, utapaswa kumfanya yeye ajisikie huru na mwenye kujiamini(confortable), lakini pia mfanye ajue kuwa unampenda hatakama haujamwambia.

Kumbuka, kama utaongea nae kama rafiki, lazima awaze na ajue kuwa wewe ni mwanaume noma sana(great guy), lakini hatahisi kwamba wewe ni mwanaume unaeweza kumchangamsha au kumfurahisha. Ili kuonekana kama mwanaume anayefurahisha kwa mwanamke yeyote, inatakiwa akuone kama mtu muhimu wa kukutana nae, na ili kufanya hivyo, msukume sukume hata bega katikati ya maongezi. Lakini usizidishe sana utaishia kumboa, fanya hivyo pale tu anapoongea jambo linalochekesha au lenye utani ndani yake.

Ila usiende na kumwambia maneno ya kawaida kama “unamuonekano mzuri”, “wewe ni mzuri sana”, au maneno yenye kufanana na hayo. Inawakera sana na haioneshi utofauti na watu wengine wa mtaani. Badala yake, jaribu kuwa specific wakati unamuambia jambo fulani mnapokutana. Mwambie maneno kama “umependeza sana leo. Huo ni mtindo mpya wa nywele?”, Hayo ni maneno mazuri sana kwa mwanamke kwa sababu ni wanaume wachache sana huyatumia kwao. Kwa hiyo unavyosema “leo umekua mrembo zaidi” inamfanya ajue ni jinsi gani unamaanisha mpaka umevunja ukimya.

Kwa kumtania huko – unaweza kufanya mambo matatu. Unaweza kumshtua na kumfanya atabasamu. Unaweza kumfanya ajue kwamba wewe unamuona mtu wa tofauti sana. Au tatu, unaweza kumfanya atambue kwamba umemwona wa kuvutia sana. Kumbuka hayo yote unamfanya yeye aone ni mtu mzuri ambaye anaweza kudate na wewe.

3. Kuwa mcheshi(be funny).
Baada ya kumfanya atabasamu na kuyafurahia maongezi yako na yeye, ni muda wa kumuingia ndani zaidi kidogo. Kila mmoja wetu anamambo yake ya siri ambayo hatupendi watu wote wajue labda mtu ambaye tunamwamini sana. Ili kumfanya ajiamini kwako, unatakiwa kumfanya awe na good time sana na wewe. Sasa hatuwezi kukuambia kabisa jinsi ya kumfanya mwanamke acheke. Lakini tunaweza kukupa mambo mawili ya kutumia. Usimwambie utani wowote wakati unaongea nae. Kuwa mwenye furaha muda wote unaoongea nae.

Hii inaweza kukutatiza kidogo. Kwanza kuongea utani wa moja kwa moja kama mtu aliyekariri ni ujinga. Badala yake, ongea nae maongezi yatakayomfanya aone unamtania, na hapo naye ataanza utani.

Jitahidi kuonesha unafurahia maongezi wakati unaongea nae kama unataka kumchangamsha. Ukiwa na furaha, dunia nzima inatabasamu pamoja nawe!. Kama unatabasamu na kujisikia furaha, naye atatabasamu pia na kuwa na furaha. Lakini kama unauoga, utamfanya naye awe
mwoga(unconfortable).

4. Unaweza kumsukuma kidogo kati kati ya maongezi
Najua unaelewa ninaposema kusukumana, hii utokea mara nyingi pale mvulana na msichana wanapukua wamezoeana, kwa hiyo kuifanya na mwanamke kwa mara ya kwanza inatakiwa uwe mwangalifu na makini ili usije kuharibu. Unapofanikiwa kufanya hivyo, jitahidi isiwe kila saa maana utamkera kama nilivyosema hapo awali.

Ili uweze kufanya hivyo inatakiwa uwe wa kawaida – chukulia kama ni mtu wa kawaida japo wewe unajua ni special. Muulize alifanya nini weekend au baada ya kutoka kazini, muulize anapenda kwenda wapi akitoka out au ni mgahawa gani anaupenda au anatamani kwenda au kitu kingine chochote ambacho ni binafsi(very personal). Lazima atajua wewe unamtania mana hakuna mtu ambaye anaweza kuulizwa maswali yote hayo na hajazoea kuulizwa, hivyo lazima afunguke.
Na bila kusitaa, usisahau kuuliza hili swali.

“Hey, samahani hii ni very personal – hivi una boyfriend? Kama unaye basi jua moyo wangu utavunjika vipisivipisi zaidi ya millioni hamsini sasa hivi!”, umeona ilivyo ya kichokozi eeh?. Lakini hii hufanya maajabu!.

Lazima acheke, lakini hiyo sentensi itaweka lengo lako kwake moja kwa moja, na lazima atajua kuwa unamtaka–hahahah!. Lakini angalia usiharibu kwa kuwa kituko baada ya kukupa jibu – maana unaweza kuta anaye, na kama atakwambia anaye tabasamu. Na ongelea mada nyingine tofauti kama vile swali lililopita halikumaanisha kitu kwako. Lengo lake lazima atakuwa ashalijua, na pia utafanikiwa kumfanya awe confortable kwako.

5. Mshike.
Huu ni uwanja hatari sana, lakini ni kitu unachopaswa kujifunza kwa sababu unataka kujua jinsi ya kumchangamsha msichana, si ndiyo? Hivyo kumshika katika muda muafaka inakamilisha point ya 5 ya mambo ambayo unapaswa kuyajua wakati unataka kumfurahisha mwanamke. Kama utafanikiwa kulifanya hili kwa usahihi, utakua umejichukulia point kubwa sana.

Sasa kumshika msichana ni kama kucheza na moto. Ukiushika fasta hauwezi kusikia joto, lakini ukiushika muda mrefu utaungua! Unaona ilivyo hatari?
Unaweza kumshika bega au mikono kama tayari ushamfurahisha vya kutosha. Lakini kumbuka hili, mshike tu pale unapokua na sababu ya kumshika, mfano mshike masikio kama unayasifia masikio yake au nywele kama unazisifia nywele zake, au mfute koti lake kama kuna kauchafu hatakama hana hako kauchafu, au mshike begani kama unatembea nae barabarani/ mtaani. Kumbuka kumshika mtu ni very personal, hivyo inabidi uwe makini sana na uangalie anamuitikio gani wakati unamshika kabla haujamshika tena.

Kama unataka kujua jinsi ya kumchangamsha msichana, yatumie haya mambo matano wakati utakapokutana na mwanamke next time. Na baada ya hapo utaona ni jinsi gani unavyoweza kumfurahisha mwanamke na kumfanya ayapende maongezi yako kwa mara ya kwanza!

Sunday, October 13, 2019

WAKINA DADA MUWE MAKINI!!!

SOMA STORY FUPI YA MAPENZI YA KUHUZUNISHA YENYE MAFUNZO KWENU HASA HASA WAKINA DADA. NI STORY YA KWELI KABISA

"Nilipoingia katika mahusiano naye nilimuamini, nikampa kila kitu nilichoweza. Nakumbuka enzi zile 
nyumbani tulikuwa tuna ng’ombe, niliiba maziwa kila siku na kumpelekea kwao. Akanenepa!! Penzi letu 
likawa huru alipoanza maisha yake mwenyewe. Sikuwa najua lolote kuhusu mapenzi. Alinifundisha.
Nikaegemeza maisha yangu yote kwake. Akanifanya nikawa mtumwa wa ngono kila nikienda chumbani 
kwake. Kama haikutosha sasa akaanza kunifundisha kunywa pombe. Niliamini kuwa ndiye mume wangu 
mtarajiwa, kwa nini nikatae? Nilimkubalia kila kitu.
Alinilazimisha ngono hata nilipokuwa katika siku zangu. Kweli nilikuwa msomi na niliyajua madhara ya 
kufanya hivyo lakini sikutaka kumuudhi huyo niliyeamini kuwa ni mume wangu. Nilipenda tutumie kinga 
lakini aliipinga sana. 
Nikapata mimba ya kwanza!! Hakuwa na pesa lakini alinilazimisha niitoe. Nikaiba pesa nyumbani 
nikafanyaalivyotaka. Kwa mara yakwanza nika toa mimba. Haikuniuma sana!! Niliamini kuwa ni yeye 
atakuja kunioa na atanifichia aibu hii.
Nilitegemea sasa tutaanza kutumia kinga. Lakini hapana haikuwa hivyo. Aliendelea kunilaghai. Tayari 
aliujua udhaifu wangu. Alinishika hapa na pale. Nikishtuka tayari amefanya anavyojua. Pombe kidogo 
na nyingine kidogo. Nikazoea lakini nikawa na wahi kulewa. Akautumia udhaifu huu kunifanyia jambo 
baya lililonifanya niandike haya kwako. Akaniingilia kinyume na maumbile. Alinilawiti!! Nilishindwa 
kumshtaki popote. Nikavumilia kwa kuwa alikuwa mume wangu mtarajiwa. Mume asiyejulikana hata kwa 
wazazi.
Mchezo ule ukaendelea. Akajitetea eti hataki nipate mimba tena, hivyo hiyo ni mbinu mbadala. Najuta 
kumuamini!! Lakini huyo alikuwa mume wangu. Miaka ikapita, ule urembo wangu niliozoea kuuona 
katika kioo ukatoweka, simu za mara kwa mara kutoka kwake zikatoweka, akawa mkali sana kwangu. 
Hakutaka niende kwake. Wakati huo nilikuwa nasoma chuo. Pesa ya mkopo ikitoka ananitafuta na 
tunakuwa marafiki tena. Anasema ananipenda na atanioa. Ananilewesha na kunitumia kinyume na 
maumbile. Pesa ikiisha na mapenzi yanaisha nabaki mwenyewe katika msoto.
Sasa akaanza kubadilisha wasichana waziwazi. Ningesema nini mimi? Ninajua alishindwa kusema neno 
moja tu. Tuachane!! Nilijuatayari ameniacha!!! Afya yangu ikadolola sana, nikalazimika kwenda kupima 
hospitali. Sikuwa na virusi. Nikapewa ushauri nikautumia.
Siku zikasonga nikampata mwanaume mwingine. Huyu alikuwa ananijali sana. Nikaanza kumsahau yule 
aliyenitenda. Nilipomaliza chuo akajitambulishanyumbani na alitaka kunioa. Akanioa kweli. Maisha 
yakaanza. Mwaka wa kwanza, mwaka wa pili na hadi wa tatu. Sikuwa nabeba mimba. Mume wangu 
alikuwa mvumilivu sana, hakuwahi kunilaumu. Lakini niliumizwa na mawifi. Nikaamua kwenda hospitali.
Nikaambiwa kizazi changu kiliharibiwa kwa kutoa mimba mara kwa mara. Pia mapenzi ya kinyume na 
maumbile yamenivuruga kabisa.Nililia sana huku nikimkumbuka yule aliyeuleta uchungu huu kwangu. 
Dunia haikuwa mahali pangu sahihi. Nimekuandikia baruahii mdogo wangu. Uisome mwenyewe!! Lakini 
uwasimulie wengi baada ya kifo changu.
Uwasimulie bila kuchoka wasichana wa kileo wanaodanganyikanakufanya mambo magumu 
kuwaridhisha wapenzi wao. Waambie watakufa kwa mateso kama mimi. Wasipokusikiliza usijisikie 
vibayamaana hata mimi nilikuwa siwasikilizi watu waliponambia lolote kuhusu yule mume mdanganyifu. 
Sitajiua lakini nitakufa kabla ya wakati!!!
Nimekuandikia wewe kwa kuwa u mwandishi. Japo kwa sasa u mtoto mdogo najua utaipata nafasi siku 
moja ya kuwafikishia wasichana hawa. Usilie kwa sababu nitakufa. Lia kwasababu mwanaume 
mwenzako 

Tunakujari Kuliko unavyodhani, tunaomba Endelea kuwa sehemu yetu

Thursday, October 10, 2019

KAMA MWANUME UPO HIVI BADILIKA UNAMTESA MKE WAKO



 1.Wanaojiona Kama Wafalme (King Husband).
HIi ni aina ya wanaume ambao hutaka kusujudiwa kama wafalme na hupenda kuwafanya wake zao kuwa kama watumwa. Hawafanyi chochote ndani ya nyumba kazi yao ni kutumatuma hata kama mke anaumwa atapaswa kuamka na kupika, wanataka waheshimiwe wao tu na mwanamke akikosea kidogo ni maneno au kipigo. Mwanamke hana kauli ndani na mume akiingia nyumbani ni kama bosi anavyoingia ofisini, wote kimya hakuna hata kuongea.
2. Wanaume Wanaojihisi Bado Hawajaoa (Bachelor Husband).
Hii ni aina ya wanaume ambao hawawashirikishi wake zao kwa chochote. Hufanya mambo kama vile bado hawajaoa, hutumia muda wao mwingi na marafiki zao wakifanya mambo ambayo mke hata hayajui mke anaweza kustukizia tu mume kanunua gari bila kumshirikisha na mume haonyeshi hata kujali kuweza kumshirikisha. Hajali kama ana mke na mda mwingi huutumia akiwa na marafiki kufanya mambo yasiyo na msingi ambayo hayana mnanufaa yoyote katika ndoa yake.
3. Wanaume Wenye Gubu (Acidic Husband).
Hawa hukasirika kila mara tena bila kua na sababu ya misngi, mambo hayaishi, kosa la mwaka juzi anaweza kukukasirikia leo. Wamemuudhi kazini hataki kusemeshwa na mnanuniwa nyinyi, mwanamke akiomba hela ya chakula ni shida ni kununa kutwa nzima, wanahasira na nirahisi kumpiga mke.
4. Mume Wa Kila Mtu (Genarel Husband).
 Hawa wanajifanya wasamaria wema, wanajali kila mwanamke, wanajali marafiki wakike wa mke na wakwao kuliko wanavyowajali wake zao. Mke anaweza kuwa na shida akasema hana hela lakini rafiki akampa. Wana marafiki wengi wakike na mara nyingi huwa hawaachani kabisa na ma X wao, wakiwalalamikia wanawasaidia kuliko hata wanavyowasidia wake zao wakati wakiwa na shida.
5. Wanaume Wanaojifanya Wagumu (Dry Husband).
Hawa wanajifanya wagumu sana, hawana yale mambo ya kimahaba na wao hujua kuwa ndoa ni kuleta chakula tu na kushughulika kitandani. Hakuna kuongea na hawajali hata hisia za mke, mke akiongea kwao wala hawajali wanajifanya ni vidume sana na wanaona mambo kama vizawadi, kupiga simu, kutuma sms, kusema nakupenda, kununua maua ni mambo ya kike, yaani hawaonyeshi juhudi yoyote kuwafurahisha wekea zao.
6. Wanaume Wanaopenda Kutumia Wake Zao (Panadol Husband).
Hawa huwa wanaume pale tu wanapokuwa na shida, wanakuwa na wake wazuri wanaowajali lakini wao wala hawajali. Wanapomhitaji mwanamke, wanapotaka mwanamke awafanyie kitu flani basi huja na maneno mazuri na hata kuleta vizawadi, wanajua udhauifu wa wake zao na huutumia kuwalaghai kuwatimizia mahitaji yao lakini wanapotimiziwa tu basi husahau hata kama wanawake, hawajali tena.
7. Wanaume Ambao Hawataki Kukua (Baby Husband).
 Bado wanatabia za kitoto, hawawezi kufanya maamuzi yao wenyewe mpaka kuuliza kwa ndugu zao, mtu kaoa lakini kila siku humpigia simu Mama yake kuuliza hiki na kile. Yaani wakiongea kitu na mke nilazima aulize ndugu kwanza ndiyo kipitishwa na mke akifanya kosaa kidogo kazi nikulinganisha mke na ndugu zake, mbona flani alifanya hivi, flani anaweza fanya zaidi na mambo kama hayo. Kwakifupi hawawezi kufanya maamuzi na mkewe, ndugu zake hasa Mama yake anakuwa kama shemeu ya ndoa.
8. Mume Mtalii (Visiting Husband). 
Hawa wanakuja nyumbani kama wageni vile, mume ataihudumia familia yake kwa kila kitu lakini hawezi kuipa muda wake. Akirudi mke na watoto wamelala ni kugonga na hana sababu za msingi za kuchelewa, hata mwisho wawiki hupenda kutumia na marafiki au ndugu lakini si na mke. Hakuna kitu cha pamoja ambacho anafanya na mkewe au watoto wake, kila akiingia tu anakua na safari ya kutoka yaani hata atoke akakae nnje tu lakini si kukaa na mke au watoto.
9. Wanaume Wanaofuatilia Kila Kitu (Stalking Husband). 
Hii ni aina ya wanaume ambao hufuatilia kila kitu, huchunguza kila kitu mwanamke anachofanya na hawampi pumzi. Akienda sehemu atachunguza anaenda na nani na alikutana na nani, huwa na wivu wa ajabu ajabu na kila saa huhisi wake zao ni wasaliti. Kila mtu mwanamke anayeongea naye wa jinsia tofauti huhisi ni mchepuko na hata marafiki wa mke wakike pia huhisi wanamkuwadia, kwakifupi hampi pumzi mwanamke.
10. Mwanaume Mbahili (Miserly Husband).
Huyu anaweza kuwa na hela lakini mbahili ajabu. Akimpa mwanamke hela atafuatilia matumizi yake mpaka senti ya mwisho, anafuatilia mpaka mambo ya jikoni. Sukari ikiisha naataka ajue iliisha ishaje na kila mara huhisi mke anamuibia hela labda akajenge kwao, huwa msumbufu sana na mgumu kutoa hela. Mwanamke akifikiria mchakato wa kuomba hela kwa mume hukata tamaa na wakati mwingine kuamua tu kukaa kimya na matatizo yake.

tunakukumbusha nenda Playstore andika mchongo mpya kisha update app hii, ili ufurahie mambo mapya tuliyoyaongeza Kwa ajili yako 

Tuesday, October 8, 2019

MAANA YA ZAWADI KWENYE MAHUSIANO

Moja ya kitu ambacho huwa hakina kipaumbele sana katika mahusiano ya kimapenzi,  kitu ambacho kinachoitwa zawadi. Lakini ukweli ni kwamba zawadi ina maana kubwa sana katika mahusiano ya kimapenzi zaidi hata udhaniavyo.
Na Katika tafiti ambazo zimewahi fanywa ni kwamba, suala zima la utoaji zawadi katika mahusiano ya kimapenzi lilimekuwa likileta hisia zaidi katika upande mmoja. Yaani hapa nikiwa na maana ya kwamba jinsia ya kike ndiyo ambayo ipo katika kusubiri zawadi kutoka kwa jinsia ya kiume. Kutoka na suala hilo ndo maana watu wengi wamekuwa hawatilii maanani suala zima la zawadi. Lakini ukweli ni kwamba kila mtu anahusika kutoa zawadi.
Huenda ukawa bado nakuacha njia panda huelewi ni zawadi gani ambayo itampendeza mpenzi wako. Wala usipate tabu afisa Mipango nipo kwa ajili yako. Ipo hivi ili kujua zawadi ambayo mwezi wako anapendezwa nayo,  Unachotakiwa kukifanya ni kwamba kwa kuwa ni mpenzi wako ni mtu wa karibu jaribu kuchunguza ni kitu gani ambacho huwa anakipendelea sana,
Baada ya kupata majibu anza kufanya uchunguzi mwingine ni kitu ambacho huwa anapenda kulizungumzia sana,  baada ya kupata majibu, majibu hayo yaweke katika halmashauri yako ya kumbukumbu. Na mwisho wa siku mnunue kitu hicho kwani ndiyo zawadi itakayompendeza.
“Pia wakati mwingine maneno yangu sio sheria unaweza inanunua zawadi ambayo kiukweli unahisi fika itampendeza mwezi wako”
Hayo ni baadhi ya mambo machache ya kuzingatia katika kufanya uchaguzi wa zawadi ya kumpa mpenzi wako. Kwani zawadi ni ishara upendo imara. Pia imeshauriwa ya kwamba zawadi ni heri iwe ile ya kudumu kwani hii hukumbukwa daima.

Pasipo kupoteza muda tuendelee kidogo kwa kuangalia japo kwa uchache umuhimu wa zawadi katika mahusiano ya ndoa.
1.Huimarisha uhusiano na kuongezeka mapenzi ya kweli
Pindi utoapo zawadi kwa mwenzi wako,  mwenzi huyo hujihisi yeye ni wa thamani sana mbele yako.  kwani zawadi kutafsiriwa na mpokeaji kama ni mtu wa thamani sana,   mtu ambaye anapendwa kweli .   hivyo pindi ufanyapo kitendo cha utoaji wa zawadi yeyote ile kwa mwenzi wako, hufanya mahusiano yenu yaimarike na si kuteteleka.
2. Humfanya mtu ajihisi yupo mahali salama.
Usishangae huo ndio ukweli, kama ulikuwa hauna kawaida ya kumpa zawadi mpenzi wako basi anza kufanya hivyo mara moja.  Kwani zawadi hutafsiwa na mpokeaji ya kwamba yupo mahali sahihi. Hivyo ili kuweza kuudumisha upendo wako na mwenzi wako jenga utaratibu wa kumpa zawadi mpenzi wako.
3. Zawadi huacha kumbukumbu.
Hakuna kitu ambacho huacha alama kubwa katika mahusiano kama zawadi. Hivi hajawahi kukutana na mtu anamwambia ya kwamba kitu hiki alinipa fulani?  Bila shaka umewahi kukutana na mtu wa aina hiyo.  Kama ndivyo hivyo amini ya kwamba zawadi huacha alama katika mahusiano.
Na ili kuacha alama hiyo, kama nilivyosema hapo awali ua kwamba zawadi ni lazima iwe ni ya kudumu. Pia kabla sijaweka nukta nikumbushe pande zote mbili mvulana na msichana ana haki ya kutoa zawadi kwa mwezi wake. Hivyo nikusihi ya kwamba ujijengee utaratibu wa kutoa zawadi kwa mwezi wako.

Tumebadili mwonekano wa app yetu,na kuongeza vitu vingi zaidi, tafadhari
BOFYA HAPA  kisha update app hii, ufurahie huduma zetu.

MFAHAMU MWANAUME MWENYE AIBU KUKWAMBIA KAMA ANAKUPENDA

Ukweli usemwe. Kila mwanamume ameumbwa kivyake. Kuna wale ambao mambo yao hupenda kuyaweka wazi na wengine ambao mambo yao hupenda kuyatia kikapuni. Kuna wale ambao hawapendi kujionyesha hadharani na kuna wale ambao mambo yao huyaweka kimbelembele.
Tukija maswala ya kutongoza, kuna mitindo tofauti tofauti ambayo wanaume hutumia ili kufanikisha lengo lao. Kuna ule msemo unaosema ‘mwenda tezi na omo marejeo ni ngamani, yaani unaweza kufuata njia tofauti tofauti kufika pahali lakini mwishowe utarudi pale pale sehemu moja, so kwa wanaume kila mmoja ana mbinu yake ya kutongoza. Usiwahi kusema kuwa mwanamume aibu hajui kutongoza akiwa na wewe, labda hio aibu yake ni moja wa mtego aliouweka spesheli wa kukunasa wewe.

So utajuaje kama mwanaume mwenye aibu amekuzimia lakini hataki kuonyesha?
1. Anaingiwa na wasiwasi akiwa na wewe
Ukiona mwanaume anaingiwa na kibaridi ama kupapatika akiwa kando yako ujue ni ishara ya kukuambia kuwa amekuzimia. Hii inatokea wakati mko pamoja halafu anaingiwa na wasiwasi mara anafanya hivi mara vile.
2. Anapenda kuulizia marafiki zako kukuhusu
Mwanaume mwenye aibu akikupenda huwa anataka kukufahamu zaidi kukuhusu. Iwapo atashindwa kuongea na wewe moja kwa moja basi ataanza kuwaulizia marafiki zake kukuhusu. Ukiona mwanaume ana tabia kama hii ya kuulizia marafiki zako, lile la kufanya nikuonyesha ishara za kuwa uko huru kuongea nayeye wakati wowote ule anapojiskia huru.
3. Anakuwa na tabia isiyoeleweka akikuona
Owk wakati mwingine inatokea ya kuwa mwanaume mwenye aibu anashindwa kustahimili kuonyesha hisia zake hivyo kujaribu kuzificha ili usiweze kuzitambua. Lakini badala ya kuzificha, huibua tabia nyingine ambazo hazina mfanano wa kwake. Usishtuke ukiona akifanyika mambo ambayo si ya kawaida manake wewe ndio chanzo kikuu cha kufanyika hivyo. Yaani utakuwa umempagawisha kiasi cha kuwa anaweza kuanza kuchora miduara kwa mchanga akitumia miguu yake.
4. Anapenda kutabasamu na wewe
Wanaume wote kawaida wakipendezwa na mwanamke huwa wanatabasamu. Lakini kwa mwanaume mwenye aibu aliyekupenda huwa tabasamu lake ni tofauti. Mara nyingi atakuwa akitabasamu lakini mara kwa mara anashindwa kukuangalia usoni. Labda anaweza kukuangalia lakini pindi utakapomuangalia yeye atajifanya anaagalia kando. Hii ni baadhi ya tabia ya wanaume wa aibu hufanya wakati anapojaribu kukupendeza.

5. Anakuwa kimya ukiwa naye
Anaweza kuwa anaongea na marafiki zake sehemu flani, lakini pindi utakapotokea ananyamaza kabisa ama kuanza kuongea maneno yasiyoeleweka. Hata usishangae iwapo atakataa kujibu salam zako kama umempata katika hali kama hii. Mara nyingi ukimkuta akiwa na maongezi na marafiki zake, atajifanya hata hakuwa akizungumza katika kuchangia maongezi.
6. Anabadilisha mwonekano wake
Ukiona kuwa mwanaume mwenye aibu ameanza kubadilisha mionekano yake kwa kuanza kuvalia nguo tofauti, mitindo mipya ya nywele nk akiwa na wewe, jua hii ni ishara ya haraka kuonyesha kuwa amekuzimia.  Kufanya hivi kwa kawaida ana makusudio ya kukuridhisha wewe. Labda anadhania ya kuwa kuna mtindo fulani ambao akiuvaa unakupendeza.
7. Anagugumiza akiongea na wewe
Mwanaume huyu hujamsikia akikwamakwama wakati anapoongea lakini ghafla unamskia akigugumiza anapoongea na wewe. Hii ni ishara ya kuonyesha kuwa anaishiwa na maneno ya kukuambia na inakuwa vigumu kwake kuyatoa ama kutafuta maneno ya kukuambia.
So ni kitu gani kinachowafanya wanaume aina hii kuwa spesho kwa mwanamke?
Kuna wanawake ambao wanapenda wanaume ambao ni wa aibu kwa kuwa hawana mambo mengi. Lakini usishangae kumwona mwanaume aina hii akikuapproach akutoe mkale bata pamoja. Pia aina hii ya wanaume itafikia wakati fulani wanaweza kukushangaza kwa kufunguka na kugundua kuwa ilikuwa tu ni baadhi ya mbinu waliyotumia kukuteka kimapenzi.

Tunakukumbusha kwamba tumebadili mwonekano wa app yetu, hivyo ili kupata vitu vingi vilivyoongezwa unatakiwa BOFYA HAPA
 kisha update app hii ufurahi zaidi

Thursday, October 3, 2019

AINA ZA WANAWAKE UNAOPASWA KUWAOGOPA!!!


Katika kuangalia tabia za wanawake, nakuja na orodha ya wanawake ambao kama mwanamume unatakiwa kukaa chonjo nao kwani watayafanya maisha yako ya mahusiano kuwa ya balaa. Labda sahizi uko katika mahusiano ya muda mrefu na mpenzi wako au saa hizi uko mbioni unatafuta, kuwa macho na aina hii ya wanawake ambao wanaweza kukuharibia ama kukuletea shida
katika mahusiano yako nao mbeleni.
                       
1. Mtumiaji

Kuna aina ya wanawake ambao wanakuona wewe kama mwanamume mzuri ili wakutumie kama chambo kuwafanikisha kimaisha. Unaweza kuwa mwanamume ambaye unauunganishi na watu wengi, ama unaweza kuwa mwanamume ambaye unapendwa na wengi. Mwanamke aina hii ataona kuwa akiwa karibu na wewe itakuwa nafasi rahisi kwake kupata connection na marafiki zako kwa urahisi.

Hii inamaana kuwa pindi mwanamke aina hii akifanikiwa kupata kile ambacho amekuwa akitafuta, bila kupoteza wakati atakutema na kukuacha kwenye giza.

2. Mwanamke asiyeomba msamaha

Huyu ni aina ya mwanamke ambaye hawezi kuomba msamaha kwa jambo lolote ambalo amefanya hata kama ni la makosa kiasi gani. Anaweza kuomba msahamaha kwa shingo upande ama aamue kunyamaza kimya tu kwa jambo alilofanya la kukwaza ama kuudhi.

 kwanza ni kuwa aina hii ya mwanamke anaogofya sana kwani mtu ambaye hakubali makosa yake si mtu mzuri wa kuishi naye hata mara moja.

3. Mlalamishi

Huyu ni aina ya mwanamke ambaye nyakati zote yeye hulalamikia kuhusu hili na lile. Yaani kwake hakuna jambo zuri ambalo limeshawahi kumfanyikia. Aidha atakuwa akilalamika kuhusu marafiki zake, maisha yake ya kila siku nk. Yaani yeye siku zote hana amani. Aina hii ya mwanamke haifai kabisa kwani ulalamishi wake wa kila siku utakuchosha kwa haraka.Lakini pia lawama hazitaishia kwenye mambo mengine tu, atakulalamikia hata wewe hata kama utamfanyia jambo zuri kiasi gani

4. Asiyejielewa

Huyu ni mwanamke ambaye haelewi anachotaka maishani. (Mtaka yote)Wakati wote yeye atakuwa anahangaika na uchaguzi wake na hajiamini na chochote ambacho anachagua. Aina hii ya mwanamke achana nayo kwa sababu wewe pia inamaanisha hayuko asilimia mia moja kama aendelee kuwa nawe au la.

Aina hii ya mwanamke mara nyingi huwa na wanaume wengi na nirahisi kwake kukuendea kinyume kimapenzi. So kama wewe unamahusiano na mwanamke aina hii aidha uachane naye fasta ama akuwache wewe wa kwanza.

5. Anayetawala na kutotosheka

Hii ni aina ya mwanamke ambaye anatarajia makuu kila wakati na hatosheki kile alicho nacho. Anapenda kutawala na kila kitu anataka kifanywe vile ambavyo anavyotaka yeye. Owk najua wanawake wanapenda wanaume ambao ni gentlemen, lakini baada ya muda mfupi utakuja kugundua kwamba aina hii ya mwanamke watakufanya bwegu muda unaposongea, yaani watakukalia kichwani na wao kujifanya mabosi.

6. Mwenye maoni ya ukashifu wakati wote

Kuwa na maoni na kukashifu si jambo baya kwani kukosoa mambo katika mahusiano ni jambo zuri katika maisha. Lakini usizidishe. Aina hii ya wanawake wanaokashifu kupitia kiasi ni wale ambao wakisema jambo fulani basi litabakia hilo hilo na hata ufanyeje hawawezi kujeuza. Aina hii ya wanawake watafanya maisha yako kuwa balaa kwani wakisema jambo flani, bila hata kufikiria wenzao.

7. Nusa Nusa

Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye haipiti siku bila kukuchunguza. Kila wakati anapopata mwanya anajaribu kukuchunguza mindoko yako. Unaweza kuwa mwaminifu kwake lakini yeye bila kutosheka lazima akuchunguze chunguze, mara aangalie simu yako, atake kujua umetoka wapi umeenda wapi, jana ulivaa nguo gani, anawauliza maswali marafiki zako kukuhusu nk. Owk aina hii ya mwanamke muogope sana kwani pia yeye haaminiki. Kila anachofanya yeye anashuku pia wewe utafanya. Hivyo mara nyingi ukiona mwanamke anashindwa kukuamini kwa uhusiano, inamaanisha kuwa pia yeye ana hilo tatizo, so ukiona mwanamke wako ana hizo tabia achana nayeye mara moja.

8. Asie na maono

Aina hii ya mwanamke inafanana karibu na ile ya asiyejielewa lakini hii ni kuwa mwanamke aina hii hana maoni kujihusu yeye mwenyewe. Ukimmuliza kitu chochote anakwambia kuwa hajui ama hana mtazamo wowote kuhusu jambo lolote. Mwanamke huyu anaweza kuonekana mwanamke mzuri mara ya kwanza kwa sababu hawezi kukupinga na chochote unachosema lakini pindi muda unaposongea utaona kuwa ataanza kuwa mzigo kwako. Aina hii ya mwanake iogope sana kwa sababu anaweza kuwa anafanya hivyo maksudi huku akiwe ameweka mtego ama anamalengo yake kibinafsi kutoka kwako. Mwanamke asiyetoa maoni kuhusu chochote unachosema ni umuogope

sana.

9. Mcheza ndondi

Hii ni aina ya mwanamke amabye anakasirika kwa haraka na akichukizwa na chochote kile ambacho kinakuja kwa akili yake ni vita. Aina hii ya mwanamke sitaigusia sababu kila mtu anajua matokeo yake.

10. Mtoto wa mama

Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye hatofanya chochote bila kuingiza wazazi wake katika maongezi yake. Aina hii ya mwanamke ni mbaya kwa sababu mwanamke aina hii hata ufanye nini lazima aingize wazazi wake ndani yake. Hii inamaanisha kuwa hawezi kuthamini

 whatsApp 0717283792
Mwl. Frank Mtaha!

Wednesday, October 2, 2019

NDOA NDOANO



NDOA nikiapo au mkataba unaoingiwa na watu wawili kwa kusudi la kuishi Pamoja maisha yote watakayo ishi Duniani.

Nindoto ya Kila kijana kuwa na Ndoa japo wengi huishia kwenye kuoa na Sio ndo.

Katika maisha ni mara nyingi utasikia mtu anasema natamani kuwa na ndoa kama ya fulani, natamani kuwa na mke kama wa fulani au mume kama wa fulani.

Je mmeshawahi kujiuliza kwa nini hao mnaowatamani wako hivyo? na unapotamani kuwa na ndoa yenye furaha kama fulani je umeshajiuliza kiwango na uvumilivu cha mke au mume wa ndoa hiyo?

Umejiuliza  imani yao kwa Mungu? Kuna watu ukiwaona unatamani maisha yao wanayo ishi lakini ukiletewa sasa hivi uishi nae nina uhakika hazitazidi siku mbili umeshamrudisha ulikomtoa tena kwa bakora.

Maisha ya mahusiano yanahitaji uvumilivu wa hali ya juu usione watu wanaishi kwa furaha ukadhani simple simple tu.

Furaha haiji pasipo kuvumiliana, furaha haipatikani kama kwako kila kitu una kasilika hata kidogo tu wewe ni vita, furaha haipatikani kama huna moyo wa kusamehe, moyo wa kusitiriana, furaha hutoipata kama moyoni hauko tayari kubeba mapungufu ya mwenza wako.

Kuna watu wanaishi kwa furaha ila wemebeba misalaba mizito ila kwakua wana hekima  wavumilivu, wanasamehe, hawahesabu mabaya, basi kila gumu kwao huwa jepesi na maisha yanasonga.

Kunakanuni chache sana za kuishi ndoa
1:Nakupenda
2:Nisamehe
3:Tusahau yaliyopita.

Chukuwa hii Kanuni huwezi kushindwa ndoa lakini pia kumbuka Mwanaume kushindwa kuishi na mwanamke ni Aibu kubwa sana.

"Enyi wanaume ishini na Wake zenu kwa Akili" hayo ni maagizo toka kwenye Biblia usiwe mpumbavu ishi kwa akili

TAMBUA AINA ZA MAHUSIANO

💝💝 *UKIANZISHA MAHUSIANO HAKIKISHA UNAJUA HATIMA YAKE KWANZA*💝💝


.........
Leo nipo kutibu majeraha ya Stress zisizo za Lazima zinazotengenezwana ukosefu wa Maarifa ya Saikolojia ya Mahusiano. *Special kwa Vijana wakike na wakiume* mlio katika Mahusiano na mtakao anzisha Mahusiano.
✍Unapo anzisha Mahusiano  na mtu, jambo la kwanza  *Hakikisha unajua haya mahusiano ni ya nini? Hatima yake niya nini?* 
Kujua hatima ya Mahusiano yako itakusaidia kujipanga, kupalilia Mahusiano au Kuvunja Mahusiano yasije kukuletea Stress za bure na kukuharibia Sifa,muda na Malengo.
✍Zipo aina  za Mahusiano yanayo anzishwa kwa lengo husika, ni muhimu kujua: *Kijana Sikia tulia kwa makini usipo kuwa makini Utaishia kuumia na kulaani wakaka au wadada.

1⃣Mahusiano ya Kujioyesha.( *Show up*) _Haya hayaendi popote ni kwa ajili ya yakujionyesha kwa watu kuwa nawe una mtu wa kukuweka busy kimahusiano_
👉Mahusiano ya mitoko zaidi, story nyingi, 
I love you nyingi ila HAKUNA NDOA.

2⃣Mahusiano ya Kutojiamini( *Partial Relationship*) _Mahusiano haya ni ya kupotezeana muda, mwanzilishi wa mahusiano,au aliye katika uhusiano Hana uhakika kama aliye naye ndo chaguo sahihi lake_ kuna wakati anaonyesha kuwa ndo yeye chaguo,kuna wakati anakuwa na wasiwasi anajivuta kama anataka asitishe ila anakosa namna ya kusitisha. *Mahusiano haya Uishia na ukaa kwenye lugha za I love you tu* hakuna Step yakuonyesha Kuna sehemu tunaelekea,umebaki muda flani tuoane, kila siku nikama ndo naanza Mahusiano.( WAWEZA ZEEKEA BURE) lugha ni nzuri ila vitendo hewa.
 

        3⃣ Mahusiano ya Ngono( *Sexual Relationship*) 
_Mahusiano haya yanadumu kwa kupena sex,lakini utumika lugha ya tutaoana kwakuwa nimejua uzuri wako,radha yako sitakuacha,lakini ukweli wake, pale mdada anapo onyesha kuhutaji Engagement kijana umzungusha,ndipo vituko uanza hata kukata mawasiliano,matusi ya uzembe wa sex uanza na hamu ya kijana kuingia katika ndoa uisha._  Hapa kama ni kijana atamtumia binti sana ila ndoa atakwepa kwepa.

4⃣Mahusiano ya Kitoto( *Childish Relationship*) _Mahusiano haya wahusika ni kama watoto wanaochezea tope na mikojo,wanatumia gharama,zawadi,muda,kuitana majina ya Mtarajiwa,kuambizana nakupenda lakini wanaweza maliza hata miaka 5 *Hakuna hatua,mipango maalumu inayoonyesha wanaingia kwenye ndoa lini* hawa uishia kuachana huku wakipendana baada ya kuona muda unasonga ila hakuna dalili ya ndoa._

5⃣Mahusuano ya Ndoa ( *Marriage Relationship*) _Haya ni Mahusiano muhimu,yenye mipango,yenye malengo,yenye heshima,yenye kulinda hisia,yenye kulinda heshima,na yenye kumtanguliza Mungu_ Hapa muhusika Kijana utoa mwelekeo wa kueekea ndoa uonyesha harakati za michakato mahususi ya kuingia katika ndoa. Wakati huo huo mdada umtia moyo mwenzake,na kumwonyesha ushirikiano wa namna inavyowezekana kuifikia ndoa.

Wasiliana nami
WhatsApp 0755444078

***Elimu kwetu ndio uwanja wa nyumbani,tunakuahidi hautochoka chakufanya mwambie  jirani yako kuhusu app ya mchongo mpya****

Monday, September 30, 2019

NIFANYE MAZOEZI NA MPENZI WANGU???


Kwanza kabisa nikukaribishe sana kwenye ukurasa huu.Hakika wewe ni wa thamani.

Mazoezi ya mwili ni jambo la muhimu sana hasa katika mahusiano yako na kuimarisha ndoa na upendo bora katika familia yako.
Hata kwa vijana ambao wapo kwenye mahusiano mazoezi ni ya muhimu sana.
Swali linakuja hivi ni vyema kufanya mazoezi na mpenzi wako??
,tunaweza kulijibu hili kwa kukwambia kwamba ni vyema kabisa na itakuza sana mahusiano yako.
Kwa mfano kipindi mnakimbia yawezekana mmoja wenu akachoka na ukamuhimiza azidi kufanya mazoezi na maneno matamu yatakayokuza uhisiano wako.
Pia itaendelea kuonyesha upendo sana hasa mkifanya mazoezi wote pamoja.Mtaweza kucheka na kupata mada zaidi za mazungumzo kuliko kuongelea nini kinaendelea instagram pekee.
Hebu chukua hatua leo hii anza kufanya mazoezi ,yana faida kubwa sana kwako na kuimarisha uhusiano wako.
       *Endelea kuwa nasi ,tunakuandalia kuchambua kwa undani zaidi kuhusu faida za mazoezi kwenye mahusiano*


Sunday, September 29, 2019

UKWELI USIOPENDWA NA WANAUME



Hapa naongea na wote wakiume au wakike, lakini hasa hasa kwa wanaume.
Huu ni ukweli ambao wanaume wengi hawaupendi na mda mwingine inawapelekea kuyumba,kwenye mahusiano.Mwanaume yupo tayari kumwambia mpenzi wake kwamba alishawahi kutoka na mwanamke flani lakini hawapendi et na mtoto wa kike umwambie ulishatoka na jamaa flani, mbaya zaidi umwambie kuwa ulikuwa unasex naye sana tu, kibaya sasa umwambie Kuwa ulishatoka na zaidi ya wanaume wawili na ulikuwa unasex nao.
Aisee dadangu hapo atakushusha thamani, atakuona malaya, atajihisi kwamba hata sasa unafanya hivyo na wanaume wengine.
Wee mwanaume hebu achana na mawazo ya kijinga hayo, wakati hata wewe umefanya huo ujinga zaidi hata ya Mpenzi wako, hebu usitutishe na ubeberu wako, jiangalie na wewe Mbona hata sasa unamdanganya dada wa watu.Unajifanya upo makini sana Kumbe muongo kabisa.
Jitahidi kusahau kumbuka hiyo ni historia tu ya yaliyotokea, basi kama hauitaki usimuulize hayo mambo mpenzi wako utapata pressure bure.Kilikuwa ni kipindi tu cha maisha na sasa ameamua kuwa na wewe, muheshimu kama anavyo kuheshimu tengeneza upendo upya hayo yamepita.

Saturday, September 28, 2019

MAONGEZI HAYA YANAFAA UKIWA NDANI NA MPENZI WAKO


Aina 8 za maongezi ya kitandani ambayo ni amaizing!
#1. Kufananisha. Hii inaweza kukushangaza, lakini kama binadamu, hupenda kujifananisha na wengine kama tunataka kufurahia kuhusu sisi wenyewe. Yalinganishe mahusiano yenu ya mapezi na mahusiano ya kimapenzi ya marafiki zenu wa chuo au kazini.
Wote mtajisikia furaha kama mahusiano yenu ni mazuri zaidi ya wengine. Na kama kuna kitu mnakitamani kutoka kwenye uhusiano wa wenzenu, wote kwa pamoja mtajikuta mnafana mabadiliko ili kuimarisha maisha yenu ya kimapenzi.
#2. Ndoto za baadae. Ongeleeni kuhusu matarajio yenu na ndoto zenu katika maisha. Maongezi ya aina hii huwafanya kuzijua ndoto za mwenzako na matarajio yake ya baadae na ni jinsi gani mnaweza kusaidiana ili kuyafikia malengo yenu. Hii inawafanya muwe karibu zaidi.
#3. Pendekeza. Jitahidi kuwa mbunifu kidogo bhanaa. Au tunasema toa comment. Kama asubuhi aliondoka akiwa na nywele salu salu mwambie, lakini kama alipendeza mbwambie. Hii itawafanya wote mtabasamu.
#4. Vitu vipya vya kujaribu wakati ujao. Usifikiri huu ni mda wa kuwaza mambo magumu katika maisha kama nlivyokuambia hapo awali. Badala yake kama kuna changamoto pendekeza njia sahihi inayoweza kulitatua hilo jambo, lakini mambo mapya katika uhusiano wenu kama kwenda honeymoon kwa ajili ya exposure na vitu vingine. Kuongelea mambo ambayo yanalenga kuboresha maisha yenu inafanya maongezi ya kitandani kuwa matamu sana.
#5. Likizo na Exposure. Hakuna kinachofanya maongezi ya kitandani kuwa matamu kama kuongelea na kupanga sehemu za kutembelea baada ya miezi minne ijayo, kwa mapumziko na mpenzi wako au kwa lengo na kubadilisha mazingira na kujifunza(exposure). Jaribu kujadii ni sehemu gani nzuri za kwenda mambo ya kufanya, na mambo mengine mazuri mnayoweza kuyafanya wakati wa likizo. Hii itawafurahisha wote na itawasukuma kujituma zaidi katika maeneo yenu ya kazi na ndoto zenu zitatimia kwa uharaka zaidi.
#6. Kumbukumbu za kimahaba(Romantic Memories). Kuongelea mapenzi yenu ni kitu kizuri kitandani. Muulize mwenzio kama anakumbuka siku ya kwanza alivyokukiss ilikuaje, kama alikua anaogopa mueleze, itamfanya akumbuke mbali na kutabasamu. Maongezi ya aina hii yataanzisha mada nyingine, hivyo hamtapungukiwa na mtajikuta mnajiona wa bahati nyie kuwa pamoja.
#7. Masumbuko ya zamani. Story za zamani ni kama movie inayosisimua na kutia hamasa(inspirational movie), sanasana pale yie wawili mnapokua mnapofanikiwa katia jambo fulani baada ya kusumbuka na kujituma sana. Je, nyie wawili mlihatarisha maisha yenu ili kufanikisha mafanikio ambayo mnayo sasa? Kuyaongelea masumbuko yenu ya zamani na matunda mnayoyachuma sasa hivi inawasaidia kupata takwimu ya mambo mliyofanikiwa na kuwapa kiu ya kufanya mengi zaidi ili kuendelea kuimarika kimaisha.
#8. Ongelea siku yako ilikuaje. Hii aina ya maongezi yanawafanya nyie kuwa karibu katika shughuli zenu za kila siku. Iongelee siku yako, uzuri wako na ubaya wake, ulichofanikiwa na changamoto zilizokukumba na jinsi ya kuzitatua hizo changamoto, na kitu kingine kizuri ambacho kinakufanya ujivuie kwa ile siku kupita.
Kadri mnavyokua mnaambiana kazi zenu za kila siku kwa uwazi, inawafanya nyie mzidi kupendana zaidi na kuwa karibu kimahusiano 

****Itakuwa na mchango wako mkubwa kama ukimwambia na mwenzako kuhusu app hii, kuna mambo meng mazuri team yetu inazidi kujipanga kukuletea******
Tunakupenda.. 

DALILI KWAMBA EX WAKO ANATAKA MRUDIANE


Dalili hizi zitaonyesha wazi kwamba mpenzi wako wa zamani anatamani mrudiane. 

  1. Anakufuatilia sana kwenye mtandao ya kijamii.Anatamani kujua kila kinachooendelea kuhusu wewe,kiasi kwamba analike pia anacomment kweli post zako za mitandaoni.
  2. Atajitahidi kutokuwa na mpenzi mwingine yaani Atajitahidi kuwa mwenyewe na kutoruhusu mapenzi na mtu mwingine akijaaminisha kwamba siku moja utamrudia. 
  3. Atakutumia msg mara kwa mara ,ataendelea kukutumia msg akikutakia siku njema, Mda mwingine atakuuliza upo wap, na maswali mengi ya kawaida lakini yote hayo akihitaji Kuendelea kukuenzi moyoni mwake.  
  4. Mara nyingi atasema kwamba amekumiss. Mara kwa mara, mpenzi wako wa zamani atakwambia kuwa amekumiss na anakukumbuka sana.Tambua kabisa huyo bado anakupenda na anatamani mrudiane.

Thursday, September 26, 2019

KAMA KWELI NI MKE BORA UTAKUWA NA SIFA HIZI


Wengi wangekuja na orodha isiyokuwa na mwisho ambayo inaeleza tofauti tofauti kuhusu tabia nzuri za mwanamke. Hapa tumekuja na orodha ya sifa nzuri na muhimu zaidi ambazo zinafaa kutumiwa kama kuwa kigezo cha kupima tabia nzuri za mwanamke.
Kwa kuwa wanawake huwa na tabia tofauti tofauti, hatuwezi kusema lazima mwanamke awe na tabia zote hizi ili asomeke kama mwanamke mwenye tabia nzuri. La. hizi ni baadhi tu ya tabia ambazo mwanamke anaweza kuwa nazo, na nyingine kutokuwa nazo na bado akaorodheshwa kuwa na tabia nzuri. Zama nami.
Baadhi ya sifa nzuri kutoka kwa mwanamke
Kusamehe
Ni vigumu kuwa katika uhusiano halafu uwe hauna moyo wa kumsamehe mpenzi wako. Kawaida katika mahusiano, huwa kuna changamoto kadhaa ambazo hujitokeza hivyo lazima uwe na tabia ya kuweza kusamehe. Hii inaweza kuanzia kukosana kwa mambo ya kinyumbani, ama mambo mengine yanayofanana.
Mwanamke mzuri ni yule ambaye ana uwezo wa kumsamehe mpenzi wake bila kuweka kinyongo. Iwapo mpenzi wako umemshika katika fumanizi nk na bado unampenda, basi jambo zuri la kufanya ni kumsamehe na kuendelea na maisha.
Msikilizaji mzuri
Mara nyingi migogoro ambayo inatokea majumbani kati ya wapenzi wawili husababishwa na kutosikilizana. Huyu akiambiwa hivi huyu anajibu hivi. Iwapo mwanamke anataka mahusiano yake yake marefu na ya kufaana, basi anapaswa kuwa msikilizaji mzuri.
Mwanamke ambaye huwa anatulia na kumsikiliza mpenzi wake, mahusiano yake na mpenzi wake huwa ya furaha zaidi ukilinganisha na ya yule ambaye hatilii maanani maoni ya mwenzake.
Mwaminifu
Hii ni kuanzia kuongea ukweli bila kudanganya hadi maswala ya chumbani. Iwapo mwanamke ana mchepuko mahali fulani ama anamwendea kinyume mpenzi wake, basi aina hii ya tabia haifai kabisa.
Sifa ya mwanamke mzuri ni ile ambayo ni ya uaminifu. Mwanamke mwaminifu kwa mpenzi wake haitofika wakati fulani ambapo atakosana na mpenziwe.
Msaidifu
Katika mahusiano, kuna wakati fulani hufika ambapo lazima wapenzi wawili wasaidiane kufanya jambo ama kutimiza kitu fulani. Hivyo mwanamke mzuri ni yule ambaye anatoa msaada wa kumsaidia mpenzi wake na jambo fulani. Mathalan inaweza kuwa kumsaidia kimawazo, kifedha ama jambo tofauti. Mwanamke mwenye tabia hii humpendeza sana mpenzi wake kwa kuwa inaonyesha ya kuwa mwanamke kama huyu ana uwezo wa kumtumikia mpenzi wake wakati ambapo anaweza kupatwa na majanga.
Mwenye imani
Kuna tabia za wanawake ambazo huwachosha wanaume, nazo ni kukosa imani. Iwapo wewe una tabia za kutokuwa na imani basi tabia kama hio unafaa kuiacha mara moja. Tabia za kutokuwa na imani ni kama vile kuharakisha jambo, kulazimisha kitu ambacho hakiwezekani nk.
Hali kadhalika, mwanamke mwenye imani ni yule ambayo ana subira. Iwapo ameambiwa na mpenzi wake kuhusu jambo fulani, basi yeye hutulia hadi kungojea matokeo yake.
Kuhamasisha
Wanaume humpenda mwanamke ambaye anatoa motisha ili kumsaidia kutimiza lengo lake. Vile vile kwa kawaida kuna wanaume ambao wanahitaji kiinua mgongo ili kutimiza mambo fulani. Hivyo wewe kama mwanamke, mara moja au nyingine unafaa kuonyesha umotisha wako kwa kumuelekeza mpenzi wako mara moja au nyingine.
Mcha Mungu
Mwanamke mcha Mungu bila shaka maisha yake huwa ya kufanikiwa. Mtu yeyote yule lazima awe mcha Mungu ili awe na sifa nzuri ya maisha katika jamii.

Heshima
Heshima haimaanishi ni kwa mpenzi wako pekee bali kwa jamii nzima. Mwanamke ambaye anapenda kugombana na majirani kila kukicha halafu ikifika jioni anamheshimu mpenzi wake hafai.
Tabia za mwanamke mzuri ni yule ambaye anaheshimu na kuishi na majirani zake vizuri bila kuwa na mivurutano yeyote ile.
Anajiamini
Mwanamke mzuri ni yule anajiamini na anaamini mahusiano yake. Mwanamke mzuri ni yule ambaye hatasikia maneno ya watu halafu akampakizia mpenzi wake. Iwapo kuna swala tata ambalo linafanyika, basi mwanamke aina hii atamwekea kikao mpenzi wake na kujaribu kumuuliza maswali na kutaka kufafanua chochote ambacho kitakuwa kinamkwaza. Mwanamke aina hii hupendwa na wanaume kwa sababu anajua ya kuwa akifanya jambo fulani basi mpenzi wake atataka kuelezewa bila kuwa na hisia zozote mbaya.
Anajua mapenzi
Ikija katika swala la mapenzi, mwanamke mzuri ni yule ambaye anaujua mwili wake vizuri, hivyo si mwoga wa kuonyesha sehemu yake ya ndani ya mapenzi. Mwanamke huyu haoni aibu ya kujaribu mitindo tofauti tofauti ya kufanya mapenzi nk.
Wanawake ambao wanajua mapenzi ni moja wapo wa sifa nzuri ambayo wanaume wanapenda.


MUULIZE MASWALI HAYA MWANAUME ULIYEKUTANA NAYE MARA YA KWANZA.


Katika mazungumzo, si mwanaume pekee anapaswa kuuliza maswali. Mwanamke pia ana nafasi ya kumuuliza maswali mwanaume.
Na kumuuliza maswali kunasaidia sana kwa sababu mwanamke atapata kujua iwapo mwanaume huyu anafaa ama ni fala tu.
Wakati ambapo unamuuliza maswali, kuna maswali ambayo unafaa kuyaepuka kuyauliza kwanza ili usionekane mgumu ama mwenye dharau. Maswali haya ni yale yanahusiana na ex wake ama kumuuliza ushauri wa mahusiano. Badala yake, maswali ambayo unaweza kuuliza kwanza ni kama vile kuuliza kama yuko single na ulitoa namba yangu wapi. Lakini pia usiingie ndani kuuliza maswali haya kwa kuwa utamfanya mwanaume atunge uongo ama aishiwe na maneno.
So, ni maswali gani ya kumuuliza mwanaume unapokutana naye mara ya kwanza?
Zama nasi!
#1 Huwa unafanya nini maishani?
Hili swali ni lazima kumuuliza mwanaume. Pia swali hili limezoeka kiasi cha kuwa limepoteza ladha. Lakini usijali, huu ni mwanzo wa mazungumzo. Kazi ni kazi. Na kama anapenda kazi yake basi atakuwa na hamu ya kueleza kila kitu kuanzia mambo anayopenda na kumchukiza akiwa kazini. Hapa utapata nafasi ya kuchagua iwapo utataka kuendelea na yeye ama ulikuwa unamngojea yule mwanaume anayefanya kazi ya uhandisi.
#2 Ulilelewa wapi?
Hili swali ni la kawaida lakini pia lina umuhimu wake. Je, alilewa mjini ama kijijini. Na kama alilelewa mji mmoja na wewe na wewe ulikuwa unataka mwanaume kutoka sehemu nyingine basi huu ni wakati mzuri wa kuwa na uamuzi mzuri.
#3 Je, wewe na wazazi wako una ukaribu kiasi gani?
Mwanaume ambaye hupenda wazazi wake pia ni rahisi yeye kukutunza na kukupenda. Hivyo mwanaume akisema kuwa haishi na wazazi wake lakini kila wikendi anaenda kuwatembelea basi huyo yuko karibu na wazazi wake. Hili ni swali unapaswa kumuuliza ili uujue msimamo wake.
#4 Ni jambo gani zaidi ambalo ushawahi kulifanya ghafla
Well, swali kama hili linaweza kuwa na majibu mengi ya ghafla. Hivyo tarajia mazungumzo kunoga zaidi. Mfano anaweza kusema alienda skuba diving, anaweza kusema kuenda kuwatch gemu England bila kupanga ama anaweza kusema kukutana na wewe leo. Hapa kutakupa nafasi ya kutambua iwapo mnafaana au la.
#5 Kama ungekuwa hauko na mimi sahizi ungekuwa unafanya nini.
Hili ni swali ambalo hupaswi kuliacha. Uliza swali hili kila wakati utakabiliana na mwanaume yeyote. Swali hili lina raha yake sababu hayo majibu utakayoyapokea ni mengi.
#6 Je huwa unafuga mnyama gani wa nyumbani (pet)
Hapa utatambua iwapo huyu mwanaume anajali au la. Kulingana na utafiti unasema ya kuwa mwanaume anayefuga mnyama nyumbani aidha paka ama mbwa ana chemchembe za kujali mtu haswa anapokuwa na uhusiano na mwanamke.
Hivyo akisema hafugi chochote si mbaya, lakini mtakuwa mumekosa hadithi nyingine ndefu ya kuzungumzia.
#7 Ni kipindi gani cha utotoni ambacho ungependa kukiangalia hadi leo.
Hii ni mbinu nzuri ya kusisimua hisia za utotoni mwake. Na pindi utakapomuuliza swali kama hili utafungua ukurasa mpya kwa kuwa atajihisi yuko karibu na wewe zaidi hivyo atafunguka zaidi kwa maswali yako. Hapa usijali kama atasema angetamani kuangalia ‘Tom and Jerry’, Tausi, ama WWF. Muhimu ni kuwa anafunguka.
#8 Ni kitu gani unachukia zaidi
Swali hili si baya kuliuliza kwa kuwa kila mtu lazima kuna jambo ambalo huchukizwa nalo. Labda nyote mnachukizwa na mlevi anayelewa chakari halafu anajaribu kuzungumza na wewe na kadhalika. So si vibaya akieleza jambo lolote lile ambalo linamchukiza. Pia utapata nafasi ya kumjua mtu tabia zake.
#9 Je unaamini kuwa kuna majini na binadamu kutoka nje ya dunia (aliens)
Hii ni mada nzuri ya kuzungumzia na wanaume kawaida hupenda mijadala kama hii.  Ni vitu ambavyo hakuna uhakika vipo ama havipo na mara nyingi watu huwa na dhana tofauti tofauti na wengine hukiri kuwa wamekabiliana navyo. Hadithi kama hizi za kutisha ni nzuri pia utapata kufahamu iwapo mwanaume unayeongea naye ni mwoga au la.
#10 Ni kitu gani ambacho kitanishangaza kuhusu wewe.
Ukikutana na mwanaume mara ya kwanza, kuna yale mambo ya kawaida ambayo unatarajia mfano jina lake, sehemu anayofanya kazi na maswali yote ambayo tumeyaorodhesha hapo ju. Lakini kuna mambo mengine ambayo unaweza kushangaa kuskia ama kujua baadae. So ni muhiimu afunguke na mapema ajieleze kabla kuingia na hisia za kumpenda.
So kufikia sasa naamini maswali uko nayo. Kama awali ulikuwa una maswali ambayo umekuwa ukimuuliza mwanaume kila mnapokutana basi yaongezee ladha kwa kutumia haya tuliyokuandikia. Sisi hapa Nesi Mapenzi tunakutakia kila la heri kufanikisha azma yako.