Wednesday, October 2, 2019

NDOA NDOANO



NDOA nikiapo au mkataba unaoingiwa na watu wawili kwa kusudi la kuishi Pamoja maisha yote watakayo ishi Duniani.

Nindoto ya Kila kijana kuwa na Ndoa japo wengi huishia kwenye kuoa na Sio ndo.

Katika maisha ni mara nyingi utasikia mtu anasema natamani kuwa na ndoa kama ya fulani, natamani kuwa na mke kama wa fulani au mume kama wa fulani.

Je mmeshawahi kujiuliza kwa nini hao mnaowatamani wako hivyo? na unapotamani kuwa na ndoa yenye furaha kama fulani je umeshajiuliza kiwango na uvumilivu cha mke au mume wa ndoa hiyo?

Umejiuliza  imani yao kwa Mungu? Kuna watu ukiwaona unatamani maisha yao wanayo ishi lakini ukiletewa sasa hivi uishi nae nina uhakika hazitazidi siku mbili umeshamrudisha ulikomtoa tena kwa bakora.

Maisha ya mahusiano yanahitaji uvumilivu wa hali ya juu usione watu wanaishi kwa furaha ukadhani simple simple tu.

Furaha haiji pasipo kuvumiliana, furaha haipatikani kama kwako kila kitu una kasilika hata kidogo tu wewe ni vita, furaha haipatikani kama huna moyo wa kusamehe, moyo wa kusitiriana, furaha hutoipata kama moyoni hauko tayari kubeba mapungufu ya mwenza wako.

Kuna watu wanaishi kwa furaha ila wemebeba misalaba mizito ila kwakua wana hekima  wavumilivu, wanasamehe, hawahesabu mabaya, basi kila gumu kwao huwa jepesi na maisha yanasonga.

Kunakanuni chache sana za kuishi ndoa
1:Nakupenda
2:Nisamehe
3:Tusahau yaliyopita.

Chukuwa hii Kanuni huwezi kushindwa ndoa lakini pia kumbuka Mwanaume kushindwa kuishi na mwanamke ni Aibu kubwa sana.

"Enyi wanaume ishini na Wake zenu kwa Akili" hayo ni maagizo toka kwenye Biblia usiwe mpumbavu ishi kwa akili

No comments:

Post a Comment