Wednesday, October 2, 2019

TAMBUA AINA ZA MAHUSIANO

πŸ’πŸ’ *UKIANZISHA MAHUSIANO HAKIKISHA UNAJUA HATIMA YAKE KWANZA*πŸ’πŸ’


.........
Leo nipo kutibu majeraha ya Stress zisizo za Lazima zinazotengenezwana ukosefu wa Maarifa ya Saikolojia ya Mahusiano. *Special kwa Vijana wakike na wakiume* mlio katika Mahusiano na mtakao anzisha Mahusiano.
✍Unapo anzisha Mahusiano  na mtu, jambo la kwanza  *Hakikisha unajua haya mahusiano ni ya nini? Hatima yake niya nini?* 
Kujua hatima ya Mahusiano yako itakusaidia kujipanga, kupalilia Mahusiano au Kuvunja Mahusiano yasije kukuletea Stress za bure na kukuharibia Sifa,muda na Malengo.
✍Zipo aina  za Mahusiano yanayo anzishwa kwa lengo husika, ni muhimu kujua: *Kijana Sikia tulia kwa makini usipo kuwa makini Utaishia kuumia na kulaani wakaka au wadada.

1⃣Mahusiano ya Kujioyesha.( *Show up*) _Haya hayaendi popote ni kwa ajili ya yakujionyesha kwa watu kuwa nawe una mtu wa kukuweka busy kimahusiano_
πŸ‘‰Mahusiano ya mitoko zaidi, story nyingi, 
I love you nyingi ila HAKUNA NDOA.

2⃣Mahusiano ya Kutojiamini( *Partial Relationship*) _Mahusiano haya ni ya kupotezeana muda, mwanzilishi wa mahusiano,au aliye katika uhusiano Hana uhakika kama aliye naye ndo chaguo sahihi lake_ kuna wakati anaonyesha kuwa ndo yeye chaguo,kuna wakati anakuwa na wasiwasi anajivuta kama anataka asitishe ila anakosa namna ya kusitisha. *Mahusiano haya Uishia na ukaa kwenye lugha za I love you tu* hakuna Step yakuonyesha Kuna sehemu tunaelekea,umebaki muda flani tuoane, kila siku nikama ndo naanza Mahusiano.( WAWEZA ZEEKEA BURE) lugha ni nzuri ila vitendo hewa.
 

        3⃣ Mahusiano ya Ngono( *Sexual Relationship*) 
_Mahusiano haya yanadumu kwa kupena sex,lakini utumika lugha ya tutaoana kwakuwa nimejua uzuri wako,radha yako sitakuacha,lakini ukweli wake, pale mdada anapo onyesha kuhutaji Engagement kijana umzungusha,ndipo vituko uanza hata kukata mawasiliano,matusi ya uzembe wa sex uanza na hamu ya kijana kuingia katika ndoa uisha._  Hapa kama ni kijana atamtumia binti sana ila ndoa atakwepa kwepa.

4⃣Mahusiano ya Kitoto( *Childish Relationship*) _Mahusiano haya wahusika ni kama watoto wanaochezea tope na mikojo,wanatumia gharama,zawadi,muda,kuitana majina ya Mtarajiwa,kuambizana nakupenda lakini wanaweza maliza hata miaka 5 *Hakuna hatua,mipango maalumu inayoonyesha wanaingia kwenye ndoa lini* hawa uishia kuachana huku wakipendana baada ya kuona muda unasonga ila hakuna dalili ya ndoa._

5⃣Mahusuano ya Ndoa ( *Marriage Relationship*) _Haya ni Mahusiano muhimu,yenye mipango,yenye malengo,yenye heshima,yenye kulinda hisia,yenye kulinda heshima,na yenye kumtanguliza Mungu_ Hapa muhusika Kijana utoa mwelekeo wa kueekea ndoa uonyesha harakati za michakato mahususi ya kuingia katika ndoa. Wakati huo huo mdada umtia moyo mwenzake,na kumwonyesha ushirikiano wa namna inavyowezekana kuifikia ndoa.

Wasiliana nami
WhatsApp 0755444078

***Elimu kwetu ndio uwanja wa nyumbani,tunakuahidi hautochoka chakufanya mwambie  jirani yako kuhusu app ya mchongo mpya****

No comments:

Post a Comment