Saturday, October 19, 2019
MANENO MATAMU KWA MWENZA WAKO
Malkia wangu, kipenzi cha moyo wangu.
Asante kwa kuja kwenye maisha yangu, na kunipa furaha na upendo uliobadilisha maisha yangu.
Kamwe siwezi usahau umuhimu wako kwangu.
Na jinsi unavyonifanya nijione mwenye bahati na nimebarikiwa kushinda yeyote yule.
Sijutii kukufahamu, sijutii kuwa wako, sijutii kukupenda, na popote nilipo najivunia kuwa wako na sitachoka kuzisema sifa zako.
Babe,
Tunaishi kwenye dunia yenye watu zaidi ya billion 7, lakini bado nafsi yangu, akili yangu, macho yangu, na moyo wangu viko kwako mrembo uliyeteka hisia zangu.
Ni wewe tu unifanyae nijihisi nimekamilika kwajinsi unavyonikubali na kuyavumilia madhaifu yangu pasipo kuchoka.
Ni wewe pekee unifanyae nihisi dunia nzima iko kiganjani mwangu, kwajinsi unavyo niheshimu na kunithamini.
Nakupenda,
Nakupenda my love na sitamani kuwa mbali nawe.
Nakupenda sana kipenzi changu, and you mean everything to me.
Honey
Nitazidi kuwa mume mwema kwako, na kuhakikisha nalilinda tabasamu lako.
Nitasimama nawe na kukusupport mpaka utimize ndoto zako.
Nitakulinda na kukupa heshima na upendo ambao Malkia wangu unaustahili.
Babe you're so damn beautiful, najisikia raha kukutazama kwajinsi unavyonivutia😍
I love you, take care sweetheart 😘😘😘
***********
Kama leo hujamwambia maneno mazuri mpenzi wako, mumeo or mkeo.
Basi usiiache siku ipite bila kumwambia maneno mazuri.
Mwambie unampenda na unathamini kiasi gani uwepo wake kwenye maisha yako.
Unaweza hisi ni ujinga, lakini always maneno matamu yatokayo kwako kwenda kwa akupendae.
Huwa yana maana kubwa sana kwake, na yatampa furaha na kumfanya ajihisi dunia yote ni yake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment