Monday, September 30, 2019

NIFANYE MAZOEZI NA MPENZI WANGU???


Kwanza kabisa nikukaribishe sana kwenye ukurasa huu.Hakika wewe ni wa thamani.

Mazoezi ya mwili ni jambo la muhimu sana hasa katika mahusiano yako na kuimarisha ndoa na upendo bora katika familia yako.
Hata kwa vijana ambao wapo kwenye mahusiano mazoezi ni ya muhimu sana.
Swali linakuja hivi ni vyema kufanya mazoezi na mpenzi wako??
,tunaweza kulijibu hili kwa kukwambia kwamba ni vyema kabisa na itakuza sana mahusiano yako.
Kwa mfano kipindi mnakimbia yawezekana mmoja wenu akachoka na ukamuhimiza azidi kufanya mazoezi na maneno matamu yatakayokuza uhisiano wako.
Pia itaendelea kuonyesha upendo sana hasa mkifanya mazoezi wote pamoja.Mtaweza kucheka na kupata mada zaidi za mazungumzo kuliko kuongelea nini kinaendelea instagram pekee.
Hebu chukua hatua leo hii anza kufanya mazoezi ,yana faida kubwa sana kwako na kuimarisha uhusiano wako.
       *Endelea kuwa nasi ,tunakuandalia kuchambua kwa undani zaidi kuhusu faida za mazoezi kwenye mahusiano*


No comments:

Post a Comment