Sunday, September 29, 2019
UKWELI USIOPENDWA NA WANAUME
Hapa naongea na wote wakiume au wakike, lakini hasa hasa kwa wanaume.
Huu ni ukweli ambao wanaume wengi hawaupendi na mda mwingine inawapelekea kuyumba,kwenye mahusiano.Mwanaume yupo tayari kumwambia mpenzi wake kwamba alishawahi kutoka na mwanamke flani lakini hawapendi et na mtoto wa kike umwambie ulishatoka na jamaa flani, mbaya zaidi umwambie kuwa ulikuwa unasex naye sana tu, kibaya sasa umwambie Kuwa ulishatoka na zaidi ya wanaume wawili na ulikuwa unasex nao.
Aisee dadangu hapo atakushusha thamani, atakuona malaya, atajihisi kwamba hata sasa unafanya hivyo na wanaume wengine.
Wee mwanaume hebu achana na mawazo ya kijinga hayo, wakati hata wewe umefanya huo ujinga zaidi hata ya Mpenzi wako, hebu usitutishe na ubeberu wako, jiangalie na wewe Mbona hata sasa unamdanganya dada wa watu.Unajifanya upo makini sana Kumbe muongo kabisa.
Jitahidi kusahau kumbuka hiyo ni historia tu ya yaliyotokea, basi kama hauitaki usimuulize hayo mambo mpenzi wako utapata pressure bure.Kilikuwa ni kipindi tu cha maisha na sasa ameamua kuwa na wewe, muheshimu kama anavyo kuheshimu tengeneza upendo upya hayo yamepita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment