Mme wangu/Mke wangu
Hili ni jina ambalo litampa picha mwenzi wako kutambua kuwa unamfikiria Sana na uko tayari kuwa naye katika safari ya maisha.
Baba wa watoto wangu/ Mama wa watoto wangu
Ukimwita hivi mpenzi wako hasa kabla hamjaingia kwenye ndoa itamfanya mwenzi wako afurahie uwepo wako katika maisha take na utashangaa jinsi mambo yatakavyokuwa yanazidi kunawiri.
Mfalme wangu/ Malkia wangu
Sikuzote ifahamike kuwa mahusiano mazuri ni pamoja na kuwepo kwa heshima, utii, unyenyekevu pasipo kuwa na hivi vitu mahusiano yatakuwa na migigoro ya ovyo ovyo kila wakati, Ni vyema kwa kuwa na utii na heshima muite mpenzi wako hili jina mfalme wangu au Malkia wangu ili na wewe uweze kufurahia mahusiano yako.
Usifikirie kupendwa tu anza kumpenda yeye onyesha jinsi gani unamthamini Kama kweli anakupenda matokeo utayaona.
No comments:
Post a Comment