Hali husababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo kuhamishwa kikazi au kwa wale wanafunzi wa chuo wanapokuwa wapenzi chuoni baada ya kumaliza masomo kila mtu anarudi kwao. Katika Hali hiyo nini cha kufanya ili kuhakikisha unalilinda penzi lako na ikumbukwe kwamba usisubiri wewe ndo utafutwe na mwenzi wako ukitaka penzi lako lidumu ni lazima ulifanyie kazi haijalishi mlo pamoja au mpo mbali na ndio maana leo nimewaletea mada inayosema mahusiano ya mbali na jinsi ya kuyalinda, nini cha kufanya,Kuna njia mbalimbali unazoweza kuzitumia ili kulinda penzi lako na njia hizo ni
MAWASILIANO
Hi ni njia ambayo itamfanya mwenzi wako aamini kuwa unampenda na unamjali, mpigie simu kwa muda unaoona na muda mzuri ni asubuhi Sana au jioni. Hapa mtashauriana kwamba miwe mnapigiana muda gani unafaa ambao utakuwa mzuri kwa ajili ya kumpigia simu poa kumtumia meseji Kama mmeshazoeshana kutumiana meseji kutwa mara tatu Yani asubuhi, mchana na usiku Basi endelea hivyo hivyo.
MUOMBEE
Kama kweli unampenda mwenzi wako na kwa Sasa yupo mbali na wewe hakikisha kila siku unamuombea kwa Mungu. Unapofanya hivyo inasaidia kulinda penzi lenu.
UAMINIFU
Uaminifu ni kitu Cha msingi Sana katika mahusiano yetu. Ikiwa upo mbali na mwenzi wako jitahidi kuwa mwaminifu kwake. Hi inasaidia kuondoa woga na vishawishi vitakavyopelekea kuuaribu mahusiano yenu kwa sababu mahusiano ya mbali yana changamoto sana. Ni vyema kuendelea kuwa waaminifu kwa kila mmja wenu.
MFUATE HUKO ALIPO
Hii ni njia ambayo unaweza kuifanya endapo mtakubaliana hasa kwa wanandoa. Mfate mpenzi wako asiwe mpweke sana.
No comments:
Post a Comment