Wednesday, September 23, 2020

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUCHAGUA MWANAMKE SAHIHI NA WA KUDUMU.







1. MCHA MUNGU
Mwanamke anayemcha Mungu atawalea watoto kwa uadilifu na maadili mema;sifa hii ni ya lazima.


2. MNYENYEKEVU
Kuwa mnyenyekevu ni jambo muhimu sana ambalo mwanamke yoyote yule atafuata maagizo ya mumewe pasipo kuibua ugomvi.


3. ASIYEPENDA STAREHE
Burudani na starehe za mara kwa mara zitamfukuza mume. Mwanaume anataka mke ambaye ijumaa jioni mwanzo wa wikiendi si kigulu na njia kwenye nyumba za marafiki zake.


4. ATAKAYESTAHIMILI MAWIMBI
Ndoa si mteremko, pesa huisha, ugonjwe hutokea, msiba huwapata, misukosuko kutoka kwa mahasidi na mivutano ya kila aina. Ni muhimu mwanamke kukuza uvumilivu kwani utahitaji Sana kukabiliana na mawimbi yatakayowakumba.


5. MWAMINIFU
Kila mwanaume anataka mke wake pekeyake . Ni muhimu mwanamke kuwa mwaminifu kwa mwanaume wake.

No comments:

Post a Comment