Thursday, September 17, 2020

DADA,MWANAUME ANAPENDA SANA SALAMU HII




Katika mahusiano ya kimapenzi sikuzote ni vyema kusalimiana, na kusalimiana kwenyewe sio zile salamu za vijana kama mambo, shwari hapana salamu za heshima ndizo zinazotakiwa. Ndio maana leo nimekuletea mada inayosema Dada, mwanaume anapenda salamu hii. Kiuhalisia mwanaume huwa anapenda sana kupewa heshima kutoka kwa mwanamke wake, haijalishi ni wanandoa au la.

Heshima ikikosekana kwenye mahusiano yoyote yanakua hayana upendo wa dhati hivyo basi ndani ya upendo huu Kuna mambo mbalimbali ya kufanya ili kuhakikisha haushuki kiwango na mahusiano yanazidi kunawiri siku hadi siku katika maisha miongoni mwa mambo hayo ni salamu hii hapa

Shikamoo mumewangu
Hii ni salamu ya heshima ambayo wanaume huwa wanapenda sana kusalimiwa na wanawake zao. Huwa wanafarijika sana. Haijalishi umemzidi umri au kakuzidi umri salamu hii mwanaume yoyote humfanya ajihisi kuwa ni wa kipekee sana kwako na kutamfanya aongeze upendo wake kwako mfano unaweza kumwambia salamu hii mnapoamka, akiwa kazini unampigia simu ama kumtumia ujumbe mfupi mfano shikamoo mumewangu, pole na kazi pia akirudi nyumbani mpe salamu hii mahusiano yenu yataimarika zaidi na zaidi na utashangaa.

No comments:

Post a Comment