Wednesday, October 7, 2020

MAHUSIANO YA MBALI NA JINSI YA KUYALINDA









Katika maisha kuna wakati inafika huna budi kumuacha mpenzi/ mume/ mke wako kutokana na kuhamia sehemu nyingine mbali na hapo.
Hali husababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo kuhamishwa kikazi au kwa wale wanafunzi wa chuo wanapokuwa wapenzi chuoni baada ya kumaliza masomo kila mtu anarudi kwao. Katika Hali hiyo nini cha kufanya ili kuhakikisha unalilinda penzi lako na ikumbukwe kwamba usisubiri wewe ndo utafutwe na mwenzi wako ukitaka penzi lako lidumu ni lazima ulifanyie kazi haijalishi mlo pamoja au mpo mbali na ndio maana leo nimewaletea mada inayosema mahusiano ya mbali na jinsi ya kuyalinda, nini cha kufanya,Kuna njia mbalimbali unazoweza kuzitumia ili kulinda penzi lako na njia hizo ni 


MAWASILIANO
Hi ni njia ambayo itamfanya mwenzi wako aamini kuwa unampenda na unamjali, mpigie simu kwa muda unaoona na muda mzuri ni asubuhi Sana au jioni. Hapa mtashauriana kwamba miwe mnapigiana muda gani unafaa ambao utakuwa mzuri kwa ajili ya kumpigia simu poa kumtumia meseji Kama mmeshazoeshana kutumiana meseji kutwa mara tatu Yani asubuhi, mchana na usiku Basi endelea hivyo hivyo.


MUOMBEE
Kama kweli unampenda mwenzi wako na kwa Sasa yupo mbali na wewe hakikisha kila siku unamuombea kwa Mungu. Unapofanya hivyo inasaidia kulinda penzi lenu.


UAMINIFU
Uaminifu ni kitu Cha msingi Sana katika mahusiano yetu. Ikiwa upo mbali na mwenzi wako jitahidi kuwa mwaminifu kwake. Hi inasaidia kuondoa woga na vishawishi vitakavyopelekea kuuaribu mahusiano yenu kwa sababu mahusiano ya mbali yana changamoto sana. Ni vyema kuendelea kuwa waaminifu kwa kila mmja wenu.


MFUATE HUKO ALIPO
Hii ni njia ambayo unaweza kuifanya endapo mtakubaliana hasa kwa wanandoa. Mfate mpenzi wako asiwe mpweke sana.

Friday, October 2, 2020

MAJINA MAZURI KWA WAPENDANAO.





Katika mahusiano Kuna mengi mazuri ya kufanya ili kuhakikisha mapenzi yenu hayashuki kiwango, hivyo basi kuna baadhi ya majina mazuri ya kumwita mpenzi wako ambayo itawasaidia kwa namna moja au nyingine kuwafikisha pale mnapopataka. Majina hayo ni;


Mme wangu/Mke wangu
Hili ni jina ambalo litampa picha mwenzi wako kutambua kuwa unamfikiria Sana na uko tayari kuwa naye katika safari ya maisha.


Baba wa watoto wangu/ Mama wa watoto wangu
Ukimwita hivi mpenzi wako hasa kabla hamjaingia kwenye ndoa itamfanya mwenzi wako afurahie uwepo wako katika maisha take na utashangaa jinsi mambo yatakavyokuwa yanazidi kunawiri.


Mfalme wangu/ Malkia wangu
Sikuzote ifahamike kuwa mahusiano mazuri ni pamoja na kuwepo kwa heshima, utii, unyenyekevu pasipo kuwa na hivi vitu mahusiano yatakuwa na migigoro ya ovyo ovyo kila wakati, Ni vyema kwa kuwa na utii na heshima muite mpenzi wako hili jina mfalme wangu au Malkia wangu ili na wewe uweze kufurahia mahusiano yako.


Usifikirie kupendwa tu anza kumpenda yeye onyesha jinsi gani unamthamini Kama kweli anakupenda matokeo utayaona.