Wednesday, September 23, 2020

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUCHAGUA MWANAMKE SAHIHI NA WA KUDUMU.







1. MCHA MUNGU
Mwanamke anayemcha Mungu atawalea watoto kwa uadilifu na maadili mema;sifa hii ni ya lazima.


2. MNYENYEKEVU
Kuwa mnyenyekevu ni jambo muhimu sana ambalo mwanamke yoyote yule atafuata maagizo ya mumewe pasipo kuibua ugomvi.


3. ASIYEPENDA STAREHE
Burudani na starehe za mara kwa mara zitamfukuza mume. Mwanaume anataka mke ambaye ijumaa jioni mwanzo wa wikiendi si kigulu na njia kwenye nyumba za marafiki zake.


4. ATAKAYESTAHIMILI MAWIMBI
Ndoa si mteremko, pesa huisha, ugonjwe hutokea, msiba huwapata, misukosuko kutoka kwa mahasidi na mivutano ya kila aina. Ni muhimu mwanamke kukuza uvumilivu kwani utahitaji Sana kukabiliana na mawimbi yatakayowakumba.


5. MWAMINIFU
Kila mwanaume anataka mke wake pekeyake . Ni muhimu mwanamke kuwa mwaminifu kwa mwanaume wake.

Thursday, September 17, 2020

DADA,MWANAUME ANAPENDA SANA SALAMU HII




Katika mahusiano ya kimapenzi sikuzote ni vyema kusalimiana, na kusalimiana kwenyewe sio zile salamu za vijana kama mambo, shwari hapana salamu za heshima ndizo zinazotakiwa. Ndio maana leo nimekuletea mada inayosema Dada, mwanaume anapenda salamu hii. Kiuhalisia mwanaume huwa anapenda sana kupewa heshima kutoka kwa mwanamke wake, haijalishi ni wanandoa au la.

Heshima ikikosekana kwenye mahusiano yoyote yanakua hayana upendo wa dhati hivyo basi ndani ya upendo huu Kuna mambo mbalimbali ya kufanya ili kuhakikisha haushuki kiwango na mahusiano yanazidi kunawiri siku hadi siku katika maisha miongoni mwa mambo hayo ni salamu hii hapa

Shikamoo mumewangu
Hii ni salamu ya heshima ambayo wanaume huwa wanapenda sana kusalimiwa na wanawake zao. Huwa wanafarijika sana. Haijalishi umemzidi umri au kakuzidi umri salamu hii mwanaume yoyote humfanya ajihisi kuwa ni wa kipekee sana kwako na kutamfanya aongeze upendo wake kwako mfano unaweza kumwambia salamu hii mnapoamka, akiwa kazini unampigia simu ama kumtumia ujumbe mfupi mfano shikamoo mumewangu, pole na kazi pia akirudi nyumbani mpe salamu hii mahusiano yenu yataimarika zaidi na zaidi na utashangaa.

Thursday, September 10, 2020

JINSI MKEO ANAVYONASA KWENYE MTEGO WA EX

Maongezi yao huwa hivi

EXπŸ‘¨πŸ»: Hellow, mambo!!?
MKEOπŸ§‘πŸ»: Poa tu, nani..?
EX πŸ‘¨πŸ»: Aah! ulifuta hadi namba yangu au sababu umeolewa?
MKEO πŸ§‘πŸ»: Hayo hayakuhusu, sema we nani..?
EXπŸ‘¨πŸ»: Mi Mcharo.
MKEO πŸ§‘πŸ»: Mungu wangu! Mzima wewe? Za siku?
EX πŸ‘¨πŸ»: Nzuri tu, nimekumiss...
MKEOπŸ§‘πŸ»: We si uliniacha bana...
EX πŸ‘¨πŸ»: Hapana, hujajua tu ninavyoumia hasa niliposikia umeolewa..
MKEO πŸ§‘πŸ»: Ndo hivyo, ninegefanyeje sasa?
EXπŸ‘¨πŸ»: Bado unaishi kwenye moyo wangu..
MKEO πŸ§‘πŸ»: Mhh!! Alaaa asante.
EX πŸ‘¨πŸ»: Nipo mkoani kwenu hapa...
MKEOπŸ§‘πŸ»: Mhh! kweli? umefikia wapi?
EXπŸ‘¨πŸ»: Nipo lodge flani huku Chuda. Nimekuja kwenye seminar mara 1..
MKEO πŸ§‘πŸ»: Haya bana karibu kwetu..
EXπŸ‘¨πŸ»: Mhh! Namuogopa mumeo.
MKEO πŸ§‘πŸ»: Hofu yako tu...
EXπŸ‘¨πŸ»:Njoo hata unisalimie jamani, nimekumiss sana.
MKEOπŸ§‘πŸ»: Mmh! Muongo mkubwa we! Wa kunimiss ntakuwa mimi?
EXπŸ‘¨πŸ»: Niamini bado nakupenda, naomba uje...
MKEOπŸ§‘πŸ»:Mhh! kutoka hapa ishu, labda kesho mume wangu akienda kazini...
EXπŸ‘¨πŸ»: Poa, saa ngapi..?
MKEOπŸ§‘πŸ»: Anaenda kazini asubuhi, hivyo mimi nitatoka mida ya saa nne hivi.
EXπŸ‘¨πŸ»: Poa, ntakuambia chumba nilichopo.
MKEOπŸ§‘πŸ»: Wee tafadhali sana babuu, siingii lodge mimi ni mke wa mtu usijisahaulishe.
EXπŸ‘¨πŸ»: Please, sitakufanya chochote...siwezi kukulazimisha usichopenda kufanya niamini.
MKEOπŸ§‘πŸ»: Wewe...ndio mnasemaga hivyo hivyo.
EX πŸ‘¨πŸ»: Please, siwezi, niamini.
MEOπŸ§‘πŸ»: Sawa lakini sitakaa sana..na ni story tu sitaki mambo mengine.
EXπŸ‘¨πŸ»: Poa, usijali my ...
MKEO πŸ§‘πŸ»: Sawa

Hivi ndivyo ma EX wanavyoharibu ndoa za watu. Mkeo akishaanza kuchat na EX WAKE..UMEKWISHA NDUGU YANGU...ni ngumu kuushinda ushawishi wa EX labda kwa mwanamke 'matured' (anayejitambua)

HIYO KESHO SASA BAADA YA KUONANA

MKEO πŸ§‘πŸ»: Ila sijapenda, uliniambia hutanifanya kitu afu umenilazimisha mpaka tumesex... sijapenda kwa kweli.
EXπŸ‘¨πŸ»: Nisamehe my.. nilishindwa si unajua tuliko toka...lakini asante nimeenjoy sana. Bado uko na utamu wako mamiii.
MKEOπŸ§‘πŸ»: Sijapenda, unadhani mume wangu akijua ntafanyaje?
EXπŸ‘¨πŸ»: Hawezi kufahamu, atajuaje sasa?
MKEOπŸ§‘πŸ»: Tambua tu hivyo..(ghafla) "usitume text amekuja.."
EXπŸ‘¨πŸ»: Poa, usiku mwema.

BAADA YA MUME KUONDOKA

MKEOπŸ§‘πŸ»: Nambie....
EXπŸ‘¨πŸ»: Poa kaondoka? 
MKEO πŸ§‘πŸ»: Ndio ila akija ntakuambia.
EXπŸ‘¨πŸ»: Poa ila mi kesho kutwa naondoka, uje uniage.
MKEOπŸ§‘πŸ»: Ntaangalia asipokuwepo.
EXπŸ‘¨πŸ»: Mhh! Jamani sasa akiwepo je?
MKEO πŸ§‘πŸ»: Mhh! Sijui ntaaga naenda kwa rafiki yangu. ntakuja ila sitakaa..
EXπŸ‘¨πŸ»: Sawa...nakupenda sana.
MKEOπŸ§‘πŸ»: Nakupenda pia..ila usirudie kuniumiza.
EXπŸ‘¨πŸ»: Sitaweza rudia tena dear..

Hivyo ndivyo mwanamke anavyoingia kwenye mtego wa ex inakuwa ngumu kuutoka. Kumbukumbu zikirudishwa nyuma ni ngumu kuepuka huu mtego. Na haya mahusiano yanaweza kudumu hata miaka 6 mume asijue...

Sasa kumbuka: ex ana mke wake, na mke wake anaweza kuwa na ex wake pia. SWALI: Je, wangapi tuko salama? VVU/UKIMWI bado upo. Ewe mwanaume ukiona dalili mbaya za mawasiliano kwa mke wako...tafadhali...usisite kufanya maamuzi ya kuokoa nafsi yako, hakika MUNGU atakuwa upande wako.

Na wewe mwanaume unayetembea na mke wa  mtu kisa, eti ni ex wako...fikiria tu mke wako anakufanyia hivyo!!  Maumivu utakayopata ndiyo anayopitia mume wa ex wako akijua. 

Waingereza wanasema "What goes round MUST come around"  hivyo hakuna ubaya unaoenda bure!! 
Kwa kiswahili twaweza sema: KILA MLA CHA MWENZIYE NA CHAKE HULIWA

πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™
Nawasilisha.