Thursday, July 30, 2020

USIMCHUKULIE EASY

FACTS ONLY...

Hakuna mwanamke wa rahisi rahisi na hakuna mwanaume mpumbavu. Mwanamke ambae umemfukuzia kwa takribani miezi 12 alilala na Boyfriend wake siku ya tatu tu baada ya kukutana.
Mwanamke ulielala nae wiki moja tu baada ya kuanza mahusiano nae ujue kuna mwanaume mwingine anamfukuzia mwaka wa pili huu na hajampata. Kama amekupenda na ameona quality anazozihitaji kwako usisimame na kusema 'she is CHEAP' au 'maharage ya Mbeya'. 

Na kwa Wanawake: Mwanaume ambae amejipinda amekununulia Iphone au chochote kile hajawahi kumnunulia hata hereni mpenzi wake wa zamani. Kama umebahatika ujue anakupenda, usidhanie kuwa yeye ni mpumbavu, mjinga au wa kumchuna.

Usimchukulie kirahisi rahisi, usimuone kama ni mjinga fulani, mtu kuwa mkarimu kwako haimaanishi ni mjinga. Wote tujifunze kuheshimu na kuzikubali zile jitihada zinazooneshwa na wenzetu katika mahusiano.

Ladies are not cheap and guys are not fool!!

Unakubaliana na hayo?

No comments:

Post a Comment