Tuesday, July 7, 2020

NASAHA BURE KWA KINA DADA


🍇Kwa nini baadhi ya wadada wanatafuta limbwata na madawa ya kuushika moyo Wa Mume wako na limbwata unayo wewe mwenyeo?

Limbwata ya kwanza:-

```🍇JICHO LAKO🍇```
Unapomuangalia mumeo lainisha jicho liwe laini na mkiongea muangalie machoni na pa kurembua urembue.

```🍇SAUTI YAKO🍇```
Ongea na mumeo kwa sauti ya upole ya kubembeleza,sauti nyororo,usiwe mropokaji hakikisha kua unaweka sauti special kwa ajili yake.

```🍇MAVAZI YAKO🍇```
Unapokua na mumeo faragha usivae madera na majuba ,vaa mavazi ya kimtego tego ,full kujiachia ,vimini ama jifunge kanga ama mtandio mwepesi.

```🍇UBUNIFU WAKO🍇```
Ubunifu kwenye mapenzi ni limbwata ya aina yake ,usifanye mazoea kwenye suala hili kila siku buni mbinu mpya,usione tabu kusoma makala za wanasaikolojia wa  mapenzi.

```🍇USAFI WAKO🍇```
Mara zote napenda kusisitiza juu ya hili ,usafi Wa chumba ,nyumba na mwili wako ,hakikisha unakua msafi mda wote kwani huwezi kujua mda gani atakuhitaji.

```🍇MANUKATO NA MAPAMBO🍇```
Unaponukia unamfanya mumeo asogee karibu yako na hakikisha kila kiungo kimevaliwa pambo lake stahiki.

```🍇MANENO MATAMU NA BASHASHA🍇```
Wadada hakuna mwanaume anaependa gubu,acha tabia ya kununa nuna ovyo,neno NAKUPENDA MUME WANGU litamke kila Mara,mkumbatie bila sababu maalum, kukumbatiana kunajenga mapenzi na kunaondosha tofauti zenu.

```🍇MAPOKEZI MAZURI NA KUMUAGA VIZURI🍇```
Jenga mazoea ya kumuaga kwa kukumbatiana na mabusu na uwe unamsindikiza na kumuombea  ,na mpokee kwa bashasha na kumpa pole ya machofu .

```🍇KULA NAE NA OGA NAE🍇```
Kuoga pamoja ni jambo jema  sana tusiiwache,na pendelea kula pamoja na kulishana kila siku.

Ukaribu wako kwake ndio limbwata itayomfanya akukumbuke popote atapokua ukijumlisha na msg za mapenzi Mara kwa Mara,hakuna mkate mgumu mbele ya supu.

🍇UKIYAPENDA YAFANYIE KAZI🍇

No comments:

Post a Comment