Tuesday, April 28, 2020
EPUKA KUWA KIPOFU KWENYE MAPENZI
Kwa kawaida binadamu anapopenda hugeuka kuwa kipofu na kiziwi juu ya yule ampendae.
Ni mgumu kuamini lolote atakalo sikia juu ya mpenzi wake.
Na ni mgumu wa kuona maovu anayofanya mpenzi wake.
Na mbaya zaidi huamini zaidi kila kitokacho ndani ya kinywa cha mpenzi wake, kiasi cha kumpumbaza na kumfanya asistukie kama anasalitiwa, anaongopewa, anatumiwa, au kupotezewa tu muda wake.
Here's a thing, usiamini kila unalosikia juu ya mpenzi wako.
Sababu sio kila lisemwalo lina ukweli ndani yake, mengine hupikwa na mahasidi kwaajili ya kuwaharibia mapenzi yenu.
Lakini pia, sio kila unalosikia kuhusu mpenzi wako basi ulidharau.
Kuwa mwepesi wa kupenda kuchunguza kwa kina, ili upate uhakika wa yale uliyoyasikia.
Hali kadhalika, kuishi ndani ya mahusiano ni sawa na kulea mtoto mdogo.
Ni jukumu la mzazi/mlezi kuchunguza kwa umakini mabadiliko ya tabia na ukuaji wa mtoto.
Vivyo hivyo kwenye mahusiano, inahitajika uwe makini kuchunguza mabadiliko ya tabia za mpenzi wako pamoja na kuwa makini kuangalia kipi kinaongezeka na kipi kinapungua katika mapenzi yenu.
Ukigundua tatizo au mabadiliko mabaya ya tabia zake, usikae kimya mpaka tatizo liote sugu.
Kaa nae chini, kemea maovu yake, mrekebishe anapokosea, muelimishe anachohitajika kukifanya.
Usifukie maovu, lalamika inapobidi, onyesha wivu wako unapohitajika.
Muonyeshe kiasi gani unampenda, ila kamwe usikubali kumuonyesha unamuamini kwa 100000% kwa kila anachofanya.
Mtu akishakugundua kwamba kwake huna usemi, unamuamini kwa kila anachokwambia.
Anaichukulia kama udhaifu wako, na kuigeuza kuwa ndio njia ya kukudanganya, kukutumia, na hata kukusaliti.
Kuwa mwepesi wa kuhoji, kuchunguza, na kukemea maovu ya mpenzi wako.
Epuka kuwa kipofu na kiziwi kwenye mapenzi.
#By_Leonard_Young_Mucky
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment