Tuesday, April 28, 2020
EPUKA KUWA KIPOFU KWENYE MAPENZI
Kwa kawaida binadamu anapopenda hugeuka kuwa kipofu na kiziwi juu ya yule ampendae.
Ni mgumu kuamini lolote atakalo sikia juu ya mpenzi wake.
Na ni mgumu wa kuona maovu anayofanya mpenzi wake.
Na mbaya zaidi huamini zaidi kila kitokacho ndani ya kinywa cha mpenzi wake, kiasi cha kumpumbaza na kumfanya asistukie kama anasalitiwa, anaongopewa, anatumiwa, au kupotezewa tu muda wake.
Here's a thing, usiamini kila unalosikia juu ya mpenzi wako.
Sababu sio kila lisemwalo lina ukweli ndani yake, mengine hupikwa na mahasidi kwaajili ya kuwaharibia mapenzi yenu.
Lakini pia, sio kila unalosikia kuhusu mpenzi wako basi ulidharau.
Kuwa mwepesi wa kupenda kuchunguza kwa kina, ili upate uhakika wa yale uliyoyasikia.
Hali kadhalika, kuishi ndani ya mahusiano ni sawa na kulea mtoto mdogo.
Ni jukumu la mzazi/mlezi kuchunguza kwa umakini mabadiliko ya tabia na ukuaji wa mtoto.
Vivyo hivyo kwenye mahusiano, inahitajika uwe makini kuchunguza mabadiliko ya tabia za mpenzi wako pamoja na kuwa makini kuangalia kipi kinaongezeka na kipi kinapungua katika mapenzi yenu.
Ukigundua tatizo au mabadiliko mabaya ya tabia zake, usikae kimya mpaka tatizo liote sugu.
Kaa nae chini, kemea maovu yake, mrekebishe anapokosea, muelimishe anachohitajika kukifanya.
Usifukie maovu, lalamika inapobidi, onyesha wivu wako unapohitajika.
Muonyeshe kiasi gani unampenda, ila kamwe usikubali kumuonyesha unamuamini kwa 100000% kwa kila anachofanya.
Mtu akishakugundua kwamba kwake huna usemi, unamuamini kwa kila anachokwambia.
Anaichukulia kama udhaifu wako, na kuigeuza kuwa ndio njia ya kukudanganya, kukutumia, na hata kukusaliti.
Kuwa mwepesi wa kuhoji, kuchunguza, na kukemea maovu ya mpenzi wako.
Epuka kuwa kipofu na kiziwi kwenye mapenzi.
#By_Leonard_Young_Mucky
Monday, April 27, 2020
UKIPATA MWANAMKE WA HIVI USIMUACHE
Oct 20, 2019 11:00 AM
Hizi ni sifa halisi za mwanamke wa kweli
1. Ni nguvu ya mwanaume
2. Ni jasiri
3. Mchapakazi
4. Mwenye kujiamini
5. Tegemeo la familia
6. Mwalimu wa watoto na familia yake kiujumla
7. Mlinzi wa mwanaume.
8. Chanzo cha baraka ya familia.
9. Adui wa maadui wa familia.
10. Sauti ya familia.
11. Mponyaji wa familia yake na taifa.
12. Mlezi wa huduma.
13. Mkombozi wa familia na taifa.
14. Msaidizi wa Mungu tumfanyie msaidizi wa kufanana naye.
15. Mwombezi wa familia, huduma na taifa.
16. Mficha siri wa Mungu
2. Ni jasiri
3. Mchapakazi
4. Mwenye kujiamini
5. Tegemeo la familia
6. Mwalimu wa watoto na familia yake kiujumla
7. Mlinzi wa mwanaume.
8. Chanzo cha baraka ya familia.
9. Adui wa maadui wa familia.
10. Sauti ya familia.
11. Mponyaji wa familia yake na taifa.
12. Mlezi wa huduma.
13. Mkombozi wa familia na taifa.
14. Msaidizi wa Mungu tumfanyie msaidizi wa kufanana naye.
15. Mwombezi wa familia, huduma na taifa.
16. Mficha siri wa Mungu
HESHIMA YA MWANAMKE KWENYE MAPENZI
Mwanamke ni kama Jua unaweza usione umuhimu wake, yaani kila siku unaenda mjini jua lipo tu, unaliangalia lakini huangalii umuhimu wake kwako. Wakati mwingine likiwa kali unaanza kulalamika kuwa linachoma na lina kera. Lakini ukitafakari kidogo tu utajua kuwa bila jua maisha yasingekuwepo.
Chakula tunachokula ni kwasababu ya Jua, mvua ikinyesha sana mafuriko yakitokea tunatamani jua, kwenye baridi tunatamani pia jua, Hatuliwazii kwasababu lipo tu na linatimiza majukumu yake kimya kimya bila kelele.
Hiyo ni sawa na mwanamke, ukishaoa kuna mambo ambayo mwanamke huyafanya na baada ya muda unaanza kuyaona ya kawaida kawaida, chakula kinakuwa mezani kila siku hujui kinapikwaje na vyombo vinaoshwaje, anabeba mimba na watoto wanazaliwa hujui maumivu aliyoyapata lakini unatabasmu na kucheka ukijisifia watoto wangu na hata mkigombana unasema niachie wanangu wewe nenda tu, utafikili unajua maumivu aloyapata kipindi anawaleta duniani hao watoto.
Watoto wanaumwa mpaka wanapona hujui hata wameponaje, wanalia usiku hujui hata nani alikuwa anawabembeleza, ukirudi unakuta nguo safi chumba kisafi hutoi hata shukurani kwakuwa ushasahau kua kuna mtu anasafisha siwe safi muda wote.
Na anafanya vitu vyote hivyo kama Jua bila kelele lakini wewe ukitoa elfu mbili ya sukari utamnyanyasia mpaka ndugu zake kuwa unawalisha wewe! Hembu siku aondoke akuachie hao watoto unaojisifia kila siku kuwa ni wakwako na kumuambia hajaja na kitu, uanze kuwapikia na kuwaandaa kwenda shule, ufue nguo zao na zako. Unaweza kuajiri mfanyakazi lakini hawezi kufanya hata nusu ya kile anachokufanyia mkeo, kwani yeye atafanya kama kazi lakini mkeo anafanya kwa mapenzi, hahitaji umlipe chochote zaidi ya kutimiza majukumu yako na kumheshimu kama mke katika maisha yenu.
Vuta picha umeamka mkeo hayupo, watoto wanataka kuogeshwa kunywa chai na kwenda shule, hapo unatakiwa kuwahi kazini na mchana watoto wale.
Mheshimu sana mkeo kuna mambo mengi ambayo anayafanya ukiambiwa uyafanye Wewe utachanganyikiwa na mkeo huyafanya kwa upendo. Mwanamke anachohitaji kwa mume ni upendo na heshima tu.
Mhudumie, mpe upendo, muheshimu na muonyeshe kuwa kwako ana umuhimu mkubwa, mfanye mkeo atabasamu kila mara na familia nzima
Sunday, April 26, 2020
UHALISIA WA NDOA ZA KIAFRIKA.
Ndoa zetu za kiAfrika zina madhaifu mengi sana.
Na madhaifu haya yanatokana na upeo wetu finyu wa kushindwa kutambua jinsi ya kuziendesha ndoa zetu katika misingi ya upendo na mapenzi ya dhati.
Tumeuendekeza mfumo dume, ubabe mbele, mapenzi nyuma.
Tumedharau yale muhimu ambayo hujenga upendo.
Najua bado hujanielewa,
Here is a thing, 90% ya wanawake walio ndani ya ndoa wapo katika stage iitwayo "Married but single".
Wapo ndani ya ndoa lakini ni kama bado wapo single.
Ana mume, lakini ni kama mume hayupo vile.
Anaishi maisha ya upweke, mume hana muda na mkewe.
Hana mapenzi na mkewe.
Kitu pekee kinachowafanya waitane mume na mke, ni kile kiapo tu walichokula na lile tendo la ndoa tu wanalofanya usiku lakini nafsi zao ziko mbalimbali.
Baada ya ndoa, asilimia kubwa ya wanaume hupunguza au hukata kabisa ukaribu, na muda wa kuwasiliana na wake zao kwa kisingizio kuwa wako busy.
Na hata wakirudi wanapunguza muda wa kukaa na kuzungumza na wake zao, kufurahi pamoja, kwa kisingizio kuwa wamechoka.
Wanadhani wako sahihi, bila kujua kuwa wanakosea, wanajiweka mbali na wake zao.
Na kuwafanya wake zao kuhisi wanasalitiwa, au hawathaminiki tena.
Na huu ndio huwa chanzo cha mwanamke kupunguza mapenzi, na mwanzo wa marumbano ndani ya nyumba.
Bila kusahau pia, wanaume wengi hawako romantic.
Hawajui wafanye nini ili kuwapa raha wake zao, kuwasisimua, na kuwajenga kihisia.
Wanadhani ni ujinga kuwa mtundu, kuwa romantic, wanasahau kuwa hiyo ndo dawa pekee ya kumteka kihisia mwanamke.
**********
Hali kadhalika kwa wanaume, dini inasema ndoa ni nusu ya pepo.
Lakini 90% ya wanaume walio ndani ya ndoa ni kama hawakupewa hiyo pepo, wanaishi ndani ya jehanamu.
Nyumbani kelele, ugomvi, stress tupu, mpaka haoni hata hamu ya kuwahi kurudi home.
Sehemu ambayo anatarajia atapata amani, upendo, na utulivu, ndipo hapo hapo anapopata kero na stress zisizoisha.
*********
Suluhisho ni moja tu,
Imeandikwa "Mwanaume na ampende mkewe".
Mwanamke anahitaji attention, anahitaji umuonyeshe ana thamani kubwa moyoni mwako.
Anahitaji muda wako, akae na wewe, azungumze na wewe.
Weka ukaribu nae, onyesha upendo na umuhimu wa uwepo wako katika maisha yake.
Usiruhusu mkeo aishi maisha ya upweke ikiwa bado unampenda, maana upweke wake utamjaza huzuni na kumchochea kujiweka karibu na wengine ambao watampa furaha na kukusahau wewe.
************
Na nyie dada zangu, hakuna kitu muhimu katika maisha ya mwanaume kama ubongo wake.
Ubongo wa mwanaume ni monotask, hauwezi kufanya vitu viwili kwa wakati mmoja.
Ndomana ukimpa stress mumeo, atajikuta anaharibu kila atakachofanya, na hata kuchochea yeye kukuchukia, au kujiweka mbali na wewe.
Au hata kushindwa kukuhudumia vizuri chumbani.
Mwanaume anahitaji utulivu, anahitaji heshima, anahitaji kujaliwa na kupewa raha na sio karaha.
********
"Mwanaume dumisha upendo kwa mkeo, na mke dumisha amani, raha na utulivu kwa mumeo. Ndoa yenu itabaki salama" - Leonard Y Mucky.
#Marriage_is_beautiful #Be_Smart
#By_Leonard_Young_Mucky
Kama bado haujaupdate app hii Basi nenda Playstore kisha update app hii utafaidi mambo mengiiiiii sana
Subscribe to:
Posts (Atom)