Friday, August 7, 2020

MAMBO MUHIMU YAKUZINGATIA UNAPOTAKA KUOA

Nmekutana na hii habari nikaona ni vizuri kushare na wanaJF ili kujenga Mjadala mpana wa haya mambo. Sifurahishwi na tabia ya leo kuoana keshi kuachana. Haipendezi kabisa. Mi nataka nikioa niwe naye hadi kifo, naamini asilimia kubwa itakuwa ni kuvumiliana..ntajitahidi kumvumilia na kumchukulia poa madhaifu yake.

Ila huyu mwenzetu kasema kabla ya kuoa Zingatia mambo haya;

1. Pata Mtu unayetaka kuingia naye kwenye Ndoa.

2. Mchunguze kama mnaendana na kukubaliana ndoto za maisha yenu.

3. Chukua muda kujua historia ya ukoo wake ili ujue ni watu wa aina gani,
=> kuna gonjwa gani linasumbua ukoo wao.

=>Je wazazi wake wamewahi kupitia talaka (Maana hiyo inaweza kuathiri philosophy yake juu ya Ndoa)

=> Mahusiano yake na Mungu yakoje? Anathamini ibada? Anazungumziaje suala la uaminifu katika kumtolea Mungu. Amempa Mungu nafasi ya ngapi?

=> Mahusiano na wazazi wake hasa Baba yake. (Mara nyingi binti asiyeheshimu mamlaka ya Baba yake na kaka zake, ni ngumu saana kuja kuheshimu Mume wake)

=> Nidhamu yake ya fedha. Hii unaweza kuichunguza mkienda outings, angalie spending ethics zake. Je ananunua kila anachokiona au kile anachokihitaji?
Je anakufikiria unavyotumia au ana-enjoy tu unavyomwaga hela?

=> Anawaza nini juu ya futute, ana mipango gani na maisha yake ya baadae. Je hiyo mipango inafanyika au ni ya kufikirika tu. (Unrealistic)

=> Anampango wa kuwa na watoto, wangapi?

=> Yuko tayari kumpa Mume wake final say kwenye maisha yake? Anakusikiliza.

Baada ya kuridhika na hayo na mengine uliyojipangia.

PANGA NDOA.

1. Panga tarehe ya kupeleka posa.

=> Fuatilia kujua utaratibu wa utamaduni wa binti unayetaka kuoa kwao wanafanyaje.

=> Baada ya Posa wanakupangia mahari.

2. Panga tarehe ya kulipa mahari.

=> Mahari itahusisha wazazi wako hivyo usitafute mahari peke yake tafuta na hela ya ziada ya kufanikisha tukio.

3. Panga tarehe ya kutangaza uchumba.
=> Ni muhimu mkishirikiana na mwenzi wako mtarajiwa.

4.Panga tarehe ya harusi na kuisimamia.

=> Yako mambo yatajitokeza kukushawishi kughairi, komaa.

Unapopanga tarehe ya harusi inakusaidia kujua ukimbizane na nini ili kufanikisha tukio. Usiseme tu nataka kuoa mwezi fulani. Ukiwa specific mwezi fulani tarehe fulani inakurahisishia kujua nini cha kuanza nacho.

MAMBO MUHIMU YA KUANDAA

Baada ya kuwa umekamilisha au umeshajua namna ya kufanikisha utaratibu wa mahari.

1. ANDAA SEHEMU MTAKAYOISHI BAADA YA HARUSI.
=> Anza kufanya adjustments ukijiandaa kuwa wawili. Kama unaweza kupanga nyumba yenye nafasi zaidi kama uwezo upo itakuwa vizuri. Maana baada ya kuoa hata wazazi wako wanaweza kukutembelea nyumbani na utapokea wageni.

2.ANDAA SUTI NA SHELA (WEDDING GOWN) ZENU.
=> Sio lazima uagize ulaya kama uwezo haupo, cha muhimu ni Ndoa harusi ni swagga tu.

3. ANDAA PETE ZA AGANO LENU.
=> Ni muhimu kuwa na pete, kama uwezo upo za dhahabu ni nzuri kwa uwezo mnaoweza kufanya. Kama uwezo haupo hata mkivaa English Gold cha msingi Ndoa ifungwe. Huko mbele Mungu atawabariki mtavaa dhahabu grade 1.

4. TENGENEZA KAMATI ITAKAYO SIMAMIA HARUSI YAKO.
=> Ipe jukumu la kuendesha shughuli ya sherehe yako.
=> Usiache kumtegemea Mungu.

5. ANDAA SHEREHE KULINGANA NA WATU WATAKAO CHANGIA.

=> Kama mpaka wiki moja kabla ya harusi una michango ya watu 50. Andaa ukumbi wa watu 70, ukizidisha hao wa familia yako na familia ya Binti tena wale muhimu tu.

Huna sababu ya kujipa stress, Ndoa ni yako.

6. USITAKE MAMBO MAKUBWA NA HUNA MFUKO WA KUYAFANYIA. FANYA UNACHOWEZA NA MUACHE MUNGU AFANYE ZIADA.

7. USIMALIZE HELA YOTE KWENYE SHEREHE NA UKAANZA MAISHA HUNA HATA HELA YA KULA.

8. JITAHIDI KUEPUKA MADENI KWA KURIDHIKA NA KINACHOWEZEKANA.

=> Harusi sio Ndoa, invest kwenye ndoa, harusi ni ya siku moja tu.

9. KUMBUKA NI MPANGO WA MUNGU WEWE KUOA HIVYO LAZIMA ATAKUSAIDIA.

10. TEGEMEA KUTOSWA/ KUACHWA NA WATU USIOTARAJIA NA TEGEMEA KUSAIDIWA NA WATU USIOTEGEMEA.

11. OMBA KULIKO ULIVYOWAHI KUOMBA MAANA NDOA NI VITA NA SHETANI HAPENDI.

12. RELAX KWASABABU YOTE YATAKUWA MAZURI MWISHO WA SIKU.

=> Ukiona umewaza mpaka mpaka unasikia kuchanganyikiwa. Zima simu, lala, usife kabla ya Ndoa. Jiepushe na Stress.

=> Siku ya Harusi tulia, hata Bibi harusi au wazazi wakichelewa jua tu unaoa na yanaisha.

13. NI MUHIMU KUWEKA SAWA NA MAMA WA MTOTO WAKO KAMA YUPO, HILI LIFANYIKE KABLA YA MCHAKATO WA HARUSI ILI ASIKULETEE ZENGWE.
=> Wengi huwa tunakuwa na mahusiano yanayo hang hewani, mtu hajui kama umeshamuacha au bado uko naye. Settle huo upumbavu kabla ya kusonga mbele.

14. HAKIKISHA UNA KAZI AU SHUGHULI YA KUWEKA CHAKULA MEZANI BAADA YA HARUSI.

Hapo tumejifunza kitu, hakikisha una Utre News app kupata mambo mazuri 

Saturday, August 1, 2020

MWANAUME MWENYE SIFA HIZI ANAKUWAGA NA MVUTO ZAIDI KATIKA MAHUSIANO YA KIMAPENZI

Hizi ni sifa muhimu sana kuwa nazo 
1. Sura Nzuri
Muonekano mzuri kwa mwanaume huwa ni kigezo cha kwanza katika maamuzi ya mwanzo kwa mwanamke lakini hata hivyo huwa ni katika mapenzi ya muda mfupi tu zaidi ya yale yanayodumu.

2. Ucheshi
Ucheshi kwa mwanaume si muhimu tu kama wenyewe bali humfanya mwanaume aonekane mwenye akili

3. Mwanaume anayetoa msaada
Wanawake hupenda wanaume wanaotoa msaada, wasio wachoyo pale wanapotafuta uhusiano wa muda mrefu

4. Utajiri/Uwezo wa kifedha
Ile imani kuwa wanaume wenye uwezo wana mvuto zaidi kwa wanawake ni kweli. Utafiti ulionesha kuwa wanawake huona wanaume wanavutia zaidi pale wanaposimama tu kwenye magari ya kifahari au nyumba, hata kama vikiwa sio vyao.

5. Umri Mkubwa
Wanawake hupenda wanaume wenye umri mkubwa kwasababu mara zote huamini kuwa wamekusanya vitu vingi na uzoefu katika maisha.

6. Ndevu
Ndevu zimekuwa zikichukuliwa kama zinazokera na kuvutia kwa wakati mmoja – yote hutegemea na mapenzi ya mtu.

7. Wagumu
Wakati utafiti wa zamani unasema kuwa wanawake huvutiwa na wanaume wanawaopenda, tafiti mpya zimedai kuwa kujifanya mgumu, kutojali kunawavutia wanawake. Kifupi, wanaweza kutaka kile wanachodhani hawawezi kupata.

8. Wanawake kwenye tamaduni zote wameonesha kuvutiwa na wanaume wanaovaa rangi nyekundu

9. Wanawake wamethibitishwa pia kuwapenda wanaume majasiri na wasiogopa