Waafrika wengi huoana ili wawe wanalala na kuamka pamoja, kuzaa watoto na kusogeza umri huku wakisubilia kifo.
1.Wanandoa wengi hupigana busu na kukumbatiana pale tu mmoja wao kapokea kitu cha thamani
2.Mume humlisha mke wake tu pale anapokuwa mgonjwa hawezi kula kwa mikono yake
3.Ukiona mwanaume anamfungulia mke wake mlango wa gari ujue mlango huo ni mbovu
4.Mwafrika kugusa shingo ya mke wake ni mpaka pale mke wake ana homa, kuja kugusa shingo tena mpaka atakapougua homa.
5.Mume kumbeba mke wake kwenye mikono yake ni pale mke anapokuwa leba anajifungua
6.Ukiona wanandoa wamekaa pamoja nje wakati wa usiku usidhani wana masuara ya kimahaba, watakuwa kunguni wamezidi wameagiza dawa ya kupulizia
7.Wanawake wengi wa kiafrika huwanunulia waume zao zawadi pale tu wanapopewa maelekezo kutoka hospitali
8.Ukiona wanandoa wanakimbia pamoja ujue wahisi hatari kila mmoja wanakimbia kuokoa uhai
9.Ukiona wanandoa wameandamana kwa pamoja ni pale wanapomfuata mzazi wa mtoto aliyegombana na mtoto wao au kwa mtu alimpa mimba mtoto wao
10.Wanandoa kuoga pamoja ni pale wote wamechelewa kazini
Wanandoa na mlio kwenye mahusiano chukueni fundisho hilo na muweze kubadilika.
Vilevile usisite kumshauri na mwenzako kupakua app hii